Hivi ndivyo unaweza kuwa bora zaidi kwenye kazi unayofanya


 

Rafiki yangu karibu sana kwenye andiko letu la leo. Katika andiko hili hapa tunaenda kuona njia nuri ya wewe kuzidi kuwa bora zaidi kwenye maisha ni kuhakikisha kwamba haurudii makosa ya uliyoyafanya jana au mwaka jana. Ukiendelea kurudia makosa yaleyale kila siku, ni wazi kuwa utaendelea kupata matokeo yaleyale. Ila ukiepuka makosa ya jana na  ukafanya vizuri zaidi leo. Basi ni wazi kuwa siku zijazo utaenda kufanya vizuri zaidi.

Kwa hiyo rafiki yangu kuanzia leo hii hakikisha kuwa unaepuka kurudia makosa ya nyuma. Kwa nini? kwa sababu umeshakutana na hayo makosa, na unajua jinsi ambavyo uliyafanya, na somo kubwa ulilopata kwenye hayo makosa. Kwa hiyo kila unapoona viashiria vya wewe kurudia hayo makosa vimeanza kujitokeza, basi jitahidi kuviepuka ili usije ukarudia hayo makosa. Nakutakia siku njema

 SOMA ZAIDI: jijengee utaratibu wa kusema kidogo na kufanya matendo makubwa.


kama bado hujajiunga na jumuiya ya wanasongambele kwenye YOUTUBE basi BONYEZA HAPA leo hii, maana kuna mengi unakosa. na hakikisha UMESUBSCRIBE

GODIUS RWEYONGEZA

MOROGORO-Tz

0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X