Hujaishi Leo Kama Hujafanya Kitu Hiki Hapa


Kheri ya siku hii ya kipekee sana. Siku ya leo napenda tu nikushirikishe kitu muhimu kwenye kuishi kwako hapa duniani. Na kitu hiki ni kuwasaidia watu.

Kiufupi ni Kuwa ukiona umepitisha siku nzima bila kufanya kitu chochote kile ambacho kinamsaidia mtu, basi ujue kuwa hujaishi ndani ya siku hiyo.

Kila siku inapaswa kuwa siku ambayo wewe hapo unaongeza thamani kwenye maisha ya watu. Hata kama ni mtu mmoja tu. Ila walau kila siku unapaswa kufanya kitu ambacho kitaongeza thamani kwa mtu. Ukiona siku nzima imeisha na wewe hujafanya kitu cha aina hiyo, basi ujue Kuwa hujaishi ndani ya hiyo siku.

Nakutakia siku njema

Godius Rweyongeza

0755848391

Morogoro-Tz

SUBSCRIBE kwenye youtube channel yangu leo kwa ajili ya kupata mafunzo muhimu. Bonyeza hapa sasa.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X