Jack Ma Afunguka: Ushauri Wake Kwa Vijana Huu Hapa


 

Vijana ndio suluhisho la kesho. Vijana wadogo ndio suluhisho kwa hofu zote. Ukikaa na vijana utakuwa mwenye nguvu muda wote. Ushauri ninaotoa kwa vijana ndio ambao naufanyia kazi mwenyewe.

Ushauri huu ni kwamba, hakuna kitu rahisi, hakuna kitu ambacho kinapatikana bure. Kama unataka kufanikiwa, unapaswa kulipa ghrama.

Alibaba imetumia miaka 18 kufikia ukubwa wa sasa. tuna bahati, lakini tunafanya kazi kwa bidii sana kuliko watu wengine.

 

Mwaka jana nilisafiri masaa 867. Hayo ni masaa ya kuwa kwenye ndege tu. Ninafanya kazi kwa bidii na watu wangu pia wanafanya kazi bidii. Kwa miaka 18 tumekuwa tukifanya kazi kama kampuni nyingine, usiku kwa mchana. Hakuna kitu kinakuja bure. Na hakuna kitu kinakuja kirahisi. Unapaswa kufikiri tofauti na unapaswa kuchukua hatua za tofauti. Kuna siku za mwanzo ambapo mawazo mbalimbali yalikuwa yanakuja kwenye meza yangu watu walipokuwa wanasema kwamba hili ni wazo la kipekee basi hilo wazo nililikuwa nalikataa.

Ila watu walipokuwa wanasema kwamba hli wazo ni gumu  kutekelezeka, basi hilo ndilo wazo ambalo nilikuwa nalikimbilia kulifanya.

 

Na mwisho, huu ni ushauri ambao pia mimi mwenyewe najiambbia kila siku, leo ni ngumu, kesho itakuwa ngumu zaidi. ila siku baada ya kesho itakuwa itakuwa nzuri. Lakini watu wengi huaga dunia kesho ioni.

Kila hatua ngumu unayopitia ni sehemu ya kujifunza.

 

Rafiki yangu kwa ushauri huo wa Jack Ma, siongezei kitu kingine. ufanyie kazi kama ambavyo ameutoa. Kila la kheri

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X