Jinsi Ya Kusoma Vitabu Vya Nakala Laini Kwa Haraka Zaidi


Tupo kwenye ulimwengu ambao umebadilika sana. kwa ssa hivi ni rahisi kumiliki maktaba kubwa kuliko maktaba ambayo aliwahi kumiliki mfalme wa karne ya 16 au 17. Hii ni kutokana na ukweli kuwa asilimia kubwa ya vitabu vinapatikana mtandaoni bure au kwa gharama ndogo.

Kutokana na mapinduzi ya kiteknlojia, basi mpaka sasa hivi tumefikia hatua ambapo tumeweza kupata aina mbili za vitabu. Vitabu ambavyo vinapasomwa kwa njia ya nakala laini (soft copy) na vitabu ambavyo vinasomwa kama nakala ngumu, (hardcopy).

Kumekuwepo na mijadala mbalimbali kutoka kwa watu, wapo wanaosema kwamba wao wanapenda kusoma nakala ngumu peke yake. Na wapo wanasema kwamba wao wangependa kusoma nakala laini peke yake. Hata hivyo mimi napendelea vitabu vya aina zote, ILA NAPENDELEA ZAIDI nakala ngumu.

Ila kutokana na urahisi wa upatikanaji, asilimia kubwa ya vitabu ninavyosoma mmi ni nakala laini.

Hivyo leo naenda kukushirikisha njia na mbinu ambazo zitakuwezesha wewe kusoma vitabu vya nakala lalini haraka zaidi ili uweze kujifunza mengi. Nimeamua nikushirikishe hili hapa kwa sababu kuna vitabu vingi vya kusoma katika karne hii. Pengine wewe unaweza kuwa unasoma kwa ajili ya kufanya utafiti, hivyo utapaswa kusoma vitabu vingi kwa wakati mmoja. Ukiwa na spidi kubwa ya usomaji

·         Itakuwezesha kusoma vitabu vingi kwa haraka

·         Itakuwezesha kupata muda wa ziada. Badala ya kusoma kurasa kumi kwa masaa matatu, utaweza kusoma kurasa hizo kwa nusu saa, huku ukipata muda wa kufanya mambo mengine kwenye maisha yako

Sasa moja kwa moja ebu tuone vitu vitakavyokusaidia wewe hapo kuwa na spidi kwenye usomaji.

 

1.       CHAGUA KITABU KIMOJA AMBACHO UTASHUGHULIKA NACHO KWA WAKATI

Ni wazi kuwa kuna vitabu vingi vya kusoma. Na unaweza kuwa umeshaanza kusoma kitabu hiki hapa kikajitokeza kingine, Hivyo ni bora wewe uchague kitabu kimoja kwa wakati ambacho utashughulika nacho kwa kina. Yaani, hicho utakisoma kiundani kwelikweli.

 

Itakuwa sio vizuri kuwa unachukua kitabu hiki, unasoma na kuishai katikati, wakati huohuo unachukua kitabukingine ambacho unasoma nacho na kuishia katikati. Jijengee utaratibu ambao utakuwezesha kusoma kitabu kimoja kiundani kwa wakati. Yaani, rasilimali zako, muda wako na kila kitu utakieleza kwa hicho kitabu.

 

2.       TENGA MUDA MAALUMU WA KUSOMA KITABU CHAKO

Unapaswa kuwa na walau na nusu saa au saa zima ambalo kiuhalisia ni la kwako, na wewe unalitumia hilo kwenye kusoma kitabu chako. Na ili kujenga tabia endelevu, basi utapaswa kuwa unasoma kitabu muda ule ule kila siku. Na kwa sababu unasoma kitabu cha nakala laini, basi ni bora ukatenga zaidi muda wa asubuhi ambapo kunakuwa na utulivu wa hali ya juu na hakutakuwa na  usumbufu mkubwa.

 

3.       HAKIKISHA UNA KIFAA KIZURI CHA KUSOMEA

Vitabu vya nakala laini vinahitaji uwe na kifaa cha kusomea. Binafsi nimekuja kugundua kuwa kadiri kifaa chako kinavyokuwa kikubwa kidogo ndivyo usomaji unakuwa rahisi zaidi. Ukiwa tablet ni bora zaidi kuliko kuwa na simu janja ya kawaida. Ukiwa na kompyuta ni bora zaidi. Ila kwa kifaa chochote kile ulichonacho sasa hivi, usihofu, kitumie hichohicho kwa kutumia njia nyingine ambazo nimeeleza hapa ili uweze kupata matokeo bora.

 

4.       ONDOA MISUKOSUKO YA KUPIGIWA au notifification KWENYE KIFAA CHAKO

Kama unatumia simu kwenye kusoma kitabu, changamoto yake kubwa inakuwa ni kwenye kupigiwa, na notification za mitandaoni. Kuna njia mbalimbali unaweza kutumia kwenye hili. Binafsi napenda kuweka simu yangu kwenye mode ya DO NOT DISTURB pale ninapokuwa nasoma vitabu au naandika. Kitu hiki kinafanya hata kama mtu anakupigia usione simu yake au kama ni ujumbe ametuma hutauona na wala hautapiga kelele. Mpaka pale utakapoamua kuangalia kwa hiari yako.

Walau hii ni nzuri, sio vile unakuwa katikati ya kusoma na kitabu ndio kimeanza kunoga afu simu inaingia.

Wakati mwingine huwa naweka BIKE MODE. Ambayo huwa inazuia simu kwa kipindi kisichopungua masaa mawili, kisha baada ya hapo inaruhusu. Kwa hiyo huwa nakuta SMS tayari zimeingia au kama missed call nazikuta na ninawatufuta wale watu kwa muda wangu.

 

Kitu kingine unapaswa kujitahidi kuzima DATA wakati unasoma kitabu. Kitu hiki hapa kitazuia notification zisizo na maana kuingia wakati unasoma.

Au muda mwingine ni bora kuhakikisha kwamba hizo notififation unazifunga kabisa zisiwe zinaingia.

 

Kama una vifaa viwili. Mfano, una simu janja mbili. basi ni bora ukaamua moja iwe ya kusomea na nyingine iwe ya mawasiliano. Ile ya mawasiliano,  uiweke pembeni au uizime kabisa wakati unasoma na wakati huohuo utumie hii ya kusomea vitabu kwa ajili ya kusoma.

Kama una simu jaja pamoja na kompyuta, basi simu iwe kwa ajili ya mawasiliano na kompyuta iwe kwa ajili ya kusoma vitabu. Utatumia simu janja pale tu utakapokuwa kwenye maeneo ambapo huwezi kufungua kompyuta kama kwenye daladala au kwenye foleni unapokuwa umesuburia kukutana na mtu fulani au kupewa huduma fulani.

 

5.       MWANGA WA CHUMBA CHAKO UNA MADHARA KWENYE USOMAJI WAKO

Vifaa hivi vya kieletroniki tunavyotumia kwenye usomaji vinatoa mwanga wake. hata hivyo ni bora ukahakikisha kwamba chumba unachosomea kinakuwa na mwanga wa kutosha. Iwe wa taa ya umeme au mwanga wa jua. Kama ni usiku hakikisha kuna taa ya umeme na inaangaza vizuri ulipokaa kusoma.

Binafsi nimegundua kwamba kusomea kwenye kiza, huwa kuna madhara kwenye macho unapoamka kesho yake.

 Pengine siku nyingine nije nikuletee madhara ya kisayansi ya kusomea kwenye kiza. Kama utapenda kupata kitu cha aina hii huko mbeleni, basi weka comment yako  HAPA CHINI

 

Rafiki yangu, hizo ndizo mbinu tamo muhimu zitakazokuwezesha wewe kusoma vitabu kwa haraka na hatimaye kukuwezesha kusoma vitabu vingi. Naam, kukuongezea maarifa mengi pia. Ni wazi kuwa umepata kitu ambacho unaenda kufanyia kazi. nikutakie kila la kheri kwenye usomaji. Ikumbukwe kwamba HAITOSHI TU KUSOMA VITABU. Ila vitendo vyako vinapaswa kuwa ni vikubwa kuliko.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X