Hivi ni kitu gani ambacho huwa kinawatofautisha matajiri na masikini? Kwa nini matajiri huwa wanaendelea kuwa matajiri na masikini kuendelea kuwa masikini? Kuna kitu gani ambacho matajiri wanakijua ambacho masikini hawajui?
Kwenye kurasa za kitabu hiki unaenda kukutana na tofauti 50 kati ya matajiri na masikni ambazo kiukweli zitakuacha mdomo wazi. Kuna vitu ambavyo umekuwa unafanya kwa siku sasa ukidhani kwamba hayo ndiyo maisha ya kitajiri, ila kwenye kitabu hiki hapa utashangaa kuona kwamba vitu hivyo havipo kabisa kwenye tabia za kitajiri, na kuna vitu umekuwa hufanyi ambavyo matajiri wanafanya kila siku na tayari vitu hivyo ni sehemu ya pili ya maisha yao.
Kama unataka kuwa tajiri na kujenga utajiri ambao utadumu kwa muda mrefu, basi hauna budi kuhakikisha kwamba unajifunza misingi ya maisha ya kitajiri na kuitumia kwenye maisha yako.
Kuna kikundi ambacho huwa kinanifurahisha jinsi kinavyoshi maisha yao kila siku. Na kikundi hiki ni kikundi cha wanamziki.Mwanamziki hata kama ni mchanga huwa anahakikisha kwamba anaishi kama mwanamziki mwenye jina kubwa. Hivyo, hata kuvaa na kwake
kunakuwa kama mwanamziki mwenye jina kubwa. Na wewe pia, kuanzia leo unaweza kuanza kuishi kama tajiri.
Bila kujali kipato chako ni kiasi gani,bila kujali akaunti yako ina kiasi gani na bila kujali unamiliki nini. ukianza kuishi kama matajiri wanavyoishi, itafikia hatua ambapo na wewe utakuwa umefuata misingi yote ya kitajiri.
Yaani, ni rahisi sana. Kama unataka kuwa tajiri basi anza kuishi na kufanya kazi zako kama ambavyo matajiri wanaishi na kufanya kazi zao. Muda si mrefu utaanza kuvutia utajiri kwako na mambo yatakuwa mazuri kama upo tayari kwa ajili ya safari hii ya kitajiri basi kinachofuata ni wewe kufanyia kazi kile ambacho unaenda kusoma kwenye kurasa za kitabu hiki hapa.
Godius Rweyongeza
Utakapokuwa umemaliza kusoma kitabu hiki, usisahau kutoa maoni yako hapa chini kwenye sehemu ya maoni. Unaweza pia kunitumia ujumbe kwa whatsap kupitia namba 0755848391. Au unaweza kunitumia barua pepe kupitia songmbele.smb@gmail.com
Ungana nami kwenye mitandaoya kijamii:
YOUTUBE: BONYEZA HAPA
FACEBOOK: BONYEZA HAPA
INSTAGRAM: BONYEZA HAPA
TWITTER: BONYEZA HAPA