KITU MUHIMU KUHUSU UWEKEZAJI


 

Unaendeleaje Rafiki yangu, hongera sana kwa siku hii kipekee sana. Leo ninaenda kuzungumzia Kitu muhimu Kuhusu uwekezaji. Na Kitu hiki ni kuwa usiangalie kiasi cha fedha ambacho unawekeza sasa hivi. Hata kama kiasi unachowezekeza sasa hivi ni kidogo, wewe usihofu. Endelea kuwekeza hicho kiasi kidogo.

Kikubwa Kuhusu uwekezaji ni mwendelezo. Ukiendelea kuweka kiasi kidogo kwa muda mrefu. Ni wazi kuwa hicho kiasi kidogo sasa kitafikia hatua ambapo kitakuwa kikubwa. Ila unapaswa kuwa na mwendelezo katika utendaji kazi wako. Sio unawekeza mara moja tu, kisha wewe mwenyewe unasahau kabisa.

Au sio unakaa eti unasubiri mpaka kila Kitu kiwe tayari ndio uweze kuanza kuwekeza. Wewe wekeza hata kama una kiwango kidogo cha fedha sasa hivi?

Godius Rweyongeza

0755848391

YouTube pia kuna somo: liangalie hapa


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X