Usiende Kukutana Na Mtu Yeyote Bila Ya Kuwa Na Uhakika Wa Hili Hapa


 

Hongera sana rafiki yangu kwa siku hii ya kipekee sana. Siku ya leo ningependa nikushirikishe kitu kimoja ambacho unapaswa kukiepuka pale unapokuwa na muadi wa kukutana na mtu. Na Kitu hiki hapa, ni kwenda kukutana na huyo mtu bila ya kujua vitu anavyopendelea huyo mtu. 

Ukipata nafasi ya kukutana na mtu, basi hakikisha kuwa unajipanga na kumjua huyo mtu kiundani. Jua huwa anapendelea nini. Kama anapenda michezo basi hakikisha na wewe pia unajithidi kuwa na uelewa wa michezo, ili kwa pamoja mpate kitu ambacho mtaongea. Kama anapenda mziki hasi fuatilia baadhi ya vitu kwenye mziki, na vielewe vizuri.

Kitu hiki hapa, kitakufanya uweze kuongea na yule mtu  kiundani. Na mtaweza kuelewana zaidi.

Kama unaenda kuomba ajira. Basi ni hii kanuni ni muhimu sana. Maana bosi akiona mnaendana katika baadhi ya vitu, ni rahisi sana kukuajiri wewe kuliko kumuajiri mtu ambaye hawaendani .

Kwa hiyo, Kila unapokuwa na muadi na mtu, itumie siku moja kabla ya tukio kuhakikisha unamjua kiundani yule ambaye unaenda kukutana naye. Siku mkikutana basi mazungumzo yenu yaanzie hata kwenye kile Kitu ambacho anapenda.

Kwa mfano kama Anapenda mpira, unaweza kuanza kumuuliza kama alingalia mechi ya siku iliyotangulia.

Kama ni MSOMAJI wa vitabu basi unaweza kuanza kumashikirikisha kitu kuhusu kitabu fulani, au hata kumpa kizawadi kidogo ya kitabu kidogo, utakachokuwa umenunua kwa bei ya kawaida tu.

SASA LABDA TUJIULIZE UNAWEZA KUPATA TAARIFA ZA MTU UNAYEENDA KUKUTANA NAYE?

Njia rahisi ni kutumia mtandao wa Google, au ingia Facebook na tumia mitandao mingine kujua kiundani Kuhusu huyo mtu.

Rafiki yangu, kwa leo naishia hapo. Nikiutakie usiku mwema.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X