ACHA UTAPELI WEWE? Hivi Ndivyo Unaweza Kuondoka Kwenye Mtego Wa Kujitapeli Mwenywe Maishani Mwako


 

Jana nilikuwa naangalia TEDTALK iliyotolewa na Ashley Stahil mwaka 2014. Kwenye maongezi yake alianza kwa kutoa stori fupi jinsi siku moja alivyotekwa na baadaye watekaji wakawa wanataka fedha kutoka kwa wazazi wake.

Sasa baada ya tukio hilo lote kuisha Ashley alikuwa anajiuliza swali, hivi inawezekanaje watu wakachagua kufanya kazi kama hiyo maishani mwao. Kwa nini baadhi ya watu wachague maisha ya kuiba kitu ambacho wengine wametafuta kupata kwa jasho? Kwa nini watu wengine wachague wito wa kuwa watekaji na matapeli kwenye maisha wakati kuna vitu vingi sana kwenye maisha?

 

Wakati anaendelea na tafakari yake aligundua kitu kimoja muhimu sana ambacho siku hii ya leo ningependa nikushirikishe na kitu hiki ni kuwa watu wengi ni watekaji na matapeli binafsi wa maisha yao. Yaani, kwamba wewe unajitapeli mwenyewe. Kuna vitu ambavyo unavifanya maishani mwako ambavyo bila kipangimizi chochote vinaonesha unajitapeli.

Inawezekana hujawahi kutekwa wala kutapeliwa na mtu yeyote ambaye alichukua fedha wala mali zako, wewe mwenyewe umejiteka mara nyingi tu, na umekuwa ukifanya hivi mra nyinigi tu, na hivyo kujinyima fursa ambazo ungekuja kufurahia hapo mbeleni.

Sasa leo hii tuendelee mbele ili tuone ni kwa jinsi gani unaweza kuondoka kwenye mtego huu wa kujiteka mwenyewe. Tunaenda kutumia mbinu zilezile ambazo Ashley ameshauri kwenye TEDTALK aliyotoa.

 

MBINU YA KWANZA; UNAPASWA KUFANYA TATHIMINI BINAFSI

 

KUJIFANYIA tathimini binafsi ni kitu kigumu ukizingatia kwamba wengi wanajihurumia. Ukiachana na kujihurumia siku hizi kuna hii mitandao ya kijamii na simu janja ambazo zinachukua muda wako mara nyingi na hivyo kukufanya ushindwe kuweka nguvu zako kwenye vitu vichache ambavyo vina manufaa kwako. Kibaya zaidi linapokuja suala la tathimini binafsi ni kwamba watu wengi hawapendi kujiambia ukweli.

Ndio maana mtu anakuwa tayari kukaa na wale washikaji wake ambao watampongeza hata kama anafanya vitu vya hovyo badala ya kukaa wana watu ambao watamwambia ukweli. Hii ni hatari sana.

Kuna maswali muhimu ambayo Ashley anashauri ujiulize wakati unafanya tathimini binafsi na maswali haya ni pamoja na;

 

·         Hivi mimi ninakwama wapi?

·          Ni wapi najishikilia mwenyewe?

·         Ni kitu gani ninajua kuhusu mimi ila natamani nisingekuwa ninajua hicho kitu?

Labda upo kwenye mahusiano ambayo si sahihi?

Labda unaumwa ila unaogopa kwenda hospitali, labda unaujua ukweli fulani kuhusu maisha yako ila bado unaogopa kuufanyia kazi au kurekebisha hiyo hali. Ni kitu gani haswa unajua ambacho unatamani wewe mwenyewe usingekuwa unajua kuhusu wewe?

Katika hatua hii unapaswa kuhakikisha kwamba unauona ukweli kama ulivyo. Sio kama ambavyo ungependa wewe mwenyewe kuuona au kama ambavyo ulikuwa siku za nyuma. Uone ukweli sasa hivi kama ulivyo.

 

MBINU YA PILI; WEKA NGUVU ZAKO KWENYE KILE AMBACHO KINAKUPA UHURU KUFANYA.

 

Asilimia kubwa ya watu wanafanya vitu ambavyo hawapendi na wala haviwapi uhuru, jinasue kwenye huo mtego kwa kuhakikisha kwamba unafanya vile ambavo wewe mwenywe unapenda kufanya. Kufanya kitu ambacho hupendi kufanya ni utapeli binafsi ambao wewe mwenyewe unaufanya na unapaswa kuuepuka.

Lakini je, utajuaje kwamba nikifanya hiki kitu ninakuwa huru na nikifanya hiki ninakuwa siko huru? Ashley anashauri kuwa unapaswa kujipa zoezi la kuandika mawazo pamoja na vitu unavyofanya, kila siku kuanzia leo kwa siku 30 zinazofuata. Andika chochote kile utakachofanya au kuwaza hata kama kitaonekana cha kijinga.

 

·         Je, vinakufanya ujisikie kama unakua au ndio kwanza unajiona kama unaangamia?

·         Je, una furaha na hayo mawazo yako au kile unachofanya au ndio yanakufanya uogope?

·         Je, unapata hamasa ya kufanya kitu gani mara kwa mara na kitu gani kinkunyima hamasa?

·         Je,  ni vile ulivyokuwa unafanya vinakufanya uwe huru au ndio inaonekana kama umefungwa gerezani?n

Kama kati ya hivyo vitu vyote ulivyofanya kuna vitu ambavyo vinakupa hamasa, basi hivyo ndivyo unapaswa kuwa unafanya. maana muda pekee ambapo hakuna mtu yeyote anaweza kukutapeli ni pale ambacho unakuwa unafanya kitu kwa hamasa kutoka ndani na unapenda hicho kitu.

 

NJJIA YA TATU; NI KUJIHUSISHA NA KAZI ZAKO

 

Baada ya kuwa umeona kitu ambacho kinakupa hamasa kufanya, basi amua kukifanya hicho kitu bila kujali upo katika hali gani sasa hivi.na wala usianze kuogopa au kusubiri mpaka pale utakapokuwa tayari, wewe kifanye tu. ukiona unaanza kusubiri mpaka uwe tayari basi ujue kwamba kuna kitu unaficha. Na hii tabia ya watu wengi ambao wanaogopa kuonesha vitu vilivyo ndani yao badala yake wanasubiri mpaka pale ambapo watakuwa tayari ili waweze kuonesha ujuzi au kipaji walichonacho

Kusubiri mpaka pale utakapokuwa tayari ni barakoa ambayo watu wanavaa ili kuuficha ukweli. Hivyo, Ashley anashauri kwamba unapaswa kufanya mabadiliko binafsi. Kitu ambacho kwenye maongezi yake amekiita (YOU TURN). Yaani, achana na uoga sasa na rudi ndani yako kwa kuanza kufanya vitu kutoka ndani yako. Anza kufanya vitu ambavyo unajisikia huru kufanya.

 

Kuna utapeli mwingine ambao watu wamekuwa wanaufanya. Na utapeli huu ni utapeli wa kiuchumi. Mtu anafanya kazi kwa bidii na kujituma ila mwisho wa siku fedha zake zinapoishia yeye mwenyewe hajui.

Miaka inazidi kusogea na hakuna maendeleo yoyote yale ambayo mtu huyo anaonekana kufanya. Karibu ujipatie kitabu cha MAAJABU YA KUWEKA AKIBA ili uweze kuondokana na utapeli binafsi wa kiuchumi. Katika kitabu hiki hapa utajifunza mbinu za kuweka akiba ambazo zitakufanya uanze kununua uhuru wako binafsi. Inalipa unapokuwa na fedha ya akiba ambayo unajua kwamba hii ni fedha yangu mwenyewe na wala hakuna mtu mwingine mwenye umiliki na hiyo fedha.

Gharama ya kitabu hiki ni elfu 7 tu. unaweza kupokea nakala yako sasa hivi kupitia HAPA

https://www.getvalue.co/home/product_details/maajabu_ya_kuweka_akiba

 

Nikushukuru kwa wakati wako.

Umekuwa name,

GODIUS RWEYONGEZA

Mwandishi, mhamasishaji na mjasiliamali.

Unaweza kuwasiliana name kupitia songambele.smb@gmail.com

Au unaweza kutumia 0755848391

www.songambeleblog.blogspot.com


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X