DAKIKA 15 NA SONGAMBELE


 

 

Rafiki yangu unaendelaje? Ni vizuri sana ushukuru kwa ajili ya siku hii ya leo. Maana, kuiona siku hii ya kipekee ni jambo jema kabisa. kuna watu wengi walitamani kuiona siku ya leo ila haikuwezekana. Hivyo, tumia sekunde chache kushukuru kwa ajili ya zawadi ya siku hii ya leo.

 

Lakini pia hakikisha kwamba unaitumia vyema siku ya leo. Hakikisha kwamba unafanya kitu cha kipekee ndani ya hii siku.

 

Siku ya leo rafiki yangu, ningependa nikwambie kwamba nimekuletea fursa ya dakika 15 na songambele. Hii ni fursa ya kupata kuongea nami moja kwa moja kupitia simu kwa dakika 15 kila wikendi. Unaweza kupata nafasi hii kwa kunitumia ujumbe mfupi na kuomba kuongea nami siku ya wikendi.

Nitakupangia muda ambao tunaweza kuongea pamoja. Na ndani ya muda huu kama utakuwa na jambo ambalo ungependa tulijadili kwa pamoja, nikushauri basi tutafanya hivyo. Unaweza kuomba kuongea nami kuhusiana na masuala ya biashara, uandishi, kujenga nidhamu binafsi, changamoto ambayo unakutana nayo au kitu chochote. Ndani ya dakika hizi 15 hizi tutaongea lakini mwisho wa siku tutapata kitu cha kwenda kufanyia kazi.

Baada ya hapo tutapanga tena ni siku gani tunaweza kuongea tena. Muda huu wa maongezi utakuwa unafanyika kila wikendi. Yaani, siku ya jumamosi au jumapili. Ila wewe unapaswa kuomba nafasi hiyo mapema sana. yaani, unapaswa kutuma ujumbe wa kuomba hiyo nafasi wiki moja kabla.

 

Kwa muda huu ambao utautumia pamoja nami, utalipia kila dakika ambayo tutaitumia kuongea kwa pamoja. Na kwa kila dakika moja ambayo itapita itakuwa ni shilingi elfu moja. hivyo kwa dakika 15 utalipia elfu 15 na malipo yatafanyika kabla ya kuanza maongezi.

 

Karibu sana rafiki yangu niweze kukusaidia.

Umekuwa name, GODIUS Rweyongeza

Namba utakayotumia kuomba muadi ni 0755848391

 

P.S. ukihitaji muadi wa kuonana name moja kwa moja badala ya kuongea kwenye simu. Gharama yake itakuwa tofauti. Utalipia 2500 kwa kila dakika. na hapa utalipia kwa dakika 30 ambayo itakuwa ni sawa na 75000 kwa nusu saa.

Karibu sana nikusaidie


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X