Fanya kitu hiki hapa siku ya leo


https://www.getvalue.co/home/product_details/maajabu_series
Pata vitsbu hivi vitano kwa bei ya kitabu kimoja https://www.getvalue.co/home/product_details/maajabu_series

Habari ya siku hiii njema rafiki yangu. Hongera sana kwa siku hii ya kipekee sana

Mara nyingi sana katika maisha huwa tunakimbizana na vitu vingi sana. unaweza kukuta kwamba mtu analalamika na kulalamika juu ya hali fulani za maisha. Kwa mfano unaweza kukuta kwamba katika kila hali yeye anaona ubaya tu wa kile kinachoonekana.

 

Ndio utasikia mtu anasema maisha magumu, mara atamlalamikia fulani. Mara atamlalamikia mtu mwingnien.

Kitu kimoja cha kipekee ambacho ningependa ufahamu siku ya leo rafiki yangu ni kuwa una sababu kuwa na furaha siku ya leo. Una kila sababu za kutembea kifua mbele. Naomba sasa ukae chini na uorodeheshe vitu vitatu ambavyo unaona unapaswa kushukuru kwa kuwa navyo siku ya leo. Lakini pia, vitu ambavyo unaona wazi kuwa vitu hivi vinapaswa kuwa ni chanzo chako cha furaha. Je, umevipata hivyo vitu. Basi kuwa na furaha kwa sababu ya hivyo vitu.

Kama bado hujavipata hivyo vitu  basi naomba uangalie kwenye hivi hapa

Unapaswa kuwa na furaha leo kwa sababu unaishi. Kuna watu wengi walitamani kuwa hai leo ila haijawezekana.

Unapaswa kuwa na furaha siku ya leo kwa sababu ya watoto, wazazi, mke au mme wako na familia nzima kiujumla.

Unapaswa kuwa na furaha siku ya leo kwa sababu ya umeweza kusoma hapa na kumaliza.

Kuna vitu vingi sana ambavyo vinapaswa kukupa furaha siku ya leo.

Walau orodhesha vitatu


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X