Hivi Ndivyo Nilivyojibu Swali Nililoulizwa Kuhusu Kitabu Cha Kutoka Mpaka Kileleni


Jana nilishiriki kwenye mjadala kwenye kundi la KITABU CHAT. ambapo mada kubwa ilikuwa ni KILICHOMO NDANI KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI. Nilianza kwa kutoa utangulizi mfupi kuhusu kitabu hiki hapa cha kipekee sana.

baada ya utangulizi na maelezo machache, yalianza kuulizwa maswali. swali la kwanza kuulizwa lilikuwa ni hili hapa chini.

 “…mtu akifanya kazi huyaelekea malengo yake, ndivyo ambavyo 

malengo nayo yanavyomfuata, hatimaye mtu pamoja na 

malengo yake huweza kukutana sehemu…” haraka nimekutana na nukuu hii Godius Rweyongeza🔥🔥

Aliyeuliza swali hilo hapo alitaka kujua haswa ni ujumbe gani uliojificha nyuma ya hiyo kauli. yafuatayo ni majibu niliyotoa

hii maana yake kuwa huwezi kukaa ukiwa umebweteka na kusubiri malengo yako yaweze kutimia. Lazima uchukue hatua na kuanza kuyafanyia kazi malengo yako.

Na kadiri unavyokuwa unayafanyia kazi malengo yako, ndivyo fursa zaidi za kutimiza malengo yako zinajitokeza. Kwa jinsi hiyo unakuta kuwa hata lile lengo ambalo lilikuwa linaonekana ni kubwa basi linaanza kutimia.

Kiufupi ni kuwa kama unataka kuhamisha mlima, lazima uchukue hatua ya kuanza kutoa jiwe moja. usitegemee kupata bahati ukiwa umejifungia chumbani kwako. 

kuwa tayari kutoka nje na kuanza kazi. humuhumu katikati mambo mazuri yatatokea na hivyo kurahisisha safari ya wewe kutimiza malengo yako. Hali kama hii haiwezi kutokea endapo utakuwa umelala tu chumbani ukiwa unasubiri labda siku moja mambo yaweze kukaa vizuri.

Rafiki yangu, hivyo ndivyo nilivyojibu swali hilo hapo. 

Kupata nakala ya kitabu hiki cha kutoka sifuri mpaka kileleni wasiliana nami kupitia 0755848391 .

kila la kheri


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X