Hivi Ndivyo Unapishana Na Fedha Kwenye Zama Hizi Za Intaneti


 

 

Rafiki yangu hongera sana kwa siku hii nyingine ya kipekee sana. siku ya leo napenda nikwambie vitu ambavyo vinakufanya upishane na fedha kwenye zama hizi za intaneti na mitandao.

 

1. kudharau majukwaa ambayo unapata. Kama  unayadharau majukwaa au kuyachukukulia poa, basi ujue kwamba unapishana na fedha. Maana majukwaa ya mitandaoni ni sawa na majukwaa ya kawaida. Ukiyatumia vizuri ni wazi kuwa utavutia watu kwako ambao watakuja kwako kununua bidhaa yako au huduma yako. Na usipoyatumia viuri basi watu hao hutawaona

 

2. kuktokukwa na tovuti au blogu

Kwenye zama hizi, mtu akihitaji kitu tu, moja kwa moja anaingia mtandaoni. Basi ni vizuri uutumie mtando huu vizuri kwa kuweka vitu vya maana. Ili watu wanaokuja kutembelea mitandao wanapotafuta kitu waweze kukupata.

Kama mpaka sasa hivi hauna tovuti wala blogu, nitafute siku ya leo niweze kuksuaidia kutengeneza blogu. Piga au tume ujumbe sasa ili uweze kusaidiwa 0755848391

 

3. kutojulikana haswa ni kitu gani unafanya mtandao

Watu wanaokutafuta mtandaoni wanapaswa kukufahamu wewe kama mtaalamu. Na sio unakuwepo tu bila mwelekeo. Kama watu hawakufahamu wewe kama mtaalamu maana yake kuna sehemu unakosea. Hakikisha kwamba unajirekebisha kuanzia leo hii.

Acha watu wakufahamu wewe kama mtaaalamu.

 

4. kutokuwa na mwendelezo wa kile unachofanya.

Ni wazi nimesema kuwa unapaswa kuwa na blogu, ila kama hauna mwendelezo wa kile ambacho unafanya, ujue unafanya kazi bure. Watu watakujua kwa mara moja kisha  utwapoteza kwa sababu ya kukosa mwendelezo

 

5. uaminifu

Mtandao unafanya kwa asilimia kubwa kwa uaminifu. Asilimia kubwa ya watu ambao utakutana nao mtadaoni ni wale ambao hamjawahi kukutana. Itafikia hatua watakutumia fedha zao wakihitaji bidhaa zako, hapo sasa unapaswa kuwa mwaminifu ili uwape huduma ambayo wao wamelipia na kwa viwango vilevile

 

Nakutakia klla la kheri.

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X