Jijengee Mazingira ya kufanikiwa


Unaweza kupata kitabu hiki kwa kubonyeza HAPA


Ujue kila mazingira huwa yana aina ya kitu ambacho huwa yanavutia. Ukijijengea mazingira ya kimafanikio ujue basi mafanikio yatakufuata. Ila usipojenga mazingira ya kimafanikio basi ujue mafanikio yatakukimbia.

Ukitaka kunielewa kwenye hili hapa nataka tu kukupa mfano wa panya na mende. Kuna mazingira ambayo huwa yanavutia panya na mende. hasa yanapokuwa machafu na giza, ila mazingira yanapokuwa safi ujue kwamba panya hao hawataonekana. Huwezi kumkuta panya kwenye eneo zuri lenye kigae na mwanga wa kutosha. Ukimkuta hapo basi kwanza angalia mazingira, utagudnua kuwa kuna kitu kinakaribisha uwepo wake.

 

Vivyo hivyo kwa viumbe vingine. ili mwembe utoe matunda ni LAZIMA tuyawepo mazingira yanasapoti utoaji wa matunda. Ukiyaondoa hayo mazingira basi ujue kwamba mwembe huo utatoa matunda uliyokuwa unategemea au utatoa kidogo sana.

Kwa hiyo rafiki yangu kama unataka kufanikiwa basi hakikisha kwamba unaejenga mazingira ya kimafanikio. Yafuatayo ni mazingira muhimu unayopaswa kuanza kuyaenga.

Anza kujenga mazingira ya akili yakaaaoaaaa.

Ilishe akili yako na vitu chanya muda wote.

Jisemee maneno chanya asubuhi, mchana jioni na kila unapokutana na changamoto.

Karibisha na kaa na watu ambao ni chanya muda wote,

Jinenee maneno chanya muda wote.

Ukikaa kwenye kundi la watu ambao wanaongea maneno ambayo ni hasi basi utapaswa kuhakikisha kwamba unapata muda ambao utatumia kwenye kujidafisha akili yako maana itakuwa imepatwa na kutu.

Mafanikio yanafuata mkondo wa mafanikio,


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X