Kama Unataka Kulipwa Zaidi, Basi Fanya Hivi


Rafiki yangu unaendeleaje. leo hii ningependa nikupe mbinu ambayo itakuwezesha wewe kulipwa zaidi. na ukweli ni kuwa kama unataka kulipwa zaidi rafiki yangu basi jifunze kuhusu mauzo. 

ukiweza kuwa muuzaji mzuri basi ni wazi kuwa huwezi kulala njaa hata siku moja. ila kama haujui kuuza utalala njaa mara nyingi tu.
unaweza kushangaa na kujiiuliza hivi kuwa si bora niwe na bidhaa nzuri? ndio unapaswa kuwa na bidhaa nzuri, ila kama huwezi kuuza haitasaidia. bidhaa nzuri bila kujua kuuza vizuri utakaa nayo wewe tu.
Kwenye kitabu cha Rich Dad poor dad, mwandishi amesema kwamba kuna siku alikkutana na mwandishi mchanga ambaye alikuwa anataka kujua ni kwa jinsi gani anaweza kutengeneza fedha kupitia uandishi.
Kiyosaki akawa amemwambia kwamba anapaswa kujifunza kuuza. Kiyosaki aliendelea kukwambia yule mwandishi mchanga kuwa, mimi sio mwandishi bora ila muuzaji bora. hata ukichukua kitabu changu, hakuna sehemu utakuta imendikwa kuwa mimi ni mwandishi bora. ila imeandikwa kuwa mimi ni muuzaji bora.
kwa hiyo kitu kimoja cha kuondoka nacho siku ya leo ni kuwa unapaswa kuhakikisha unajifunza uuzaji.

Jiunge nami youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Pata vitabu vyangu kwa KUBONYEZA HAPA

Kupata makala maalumu kwa watu maalumu basi BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X