KUNA KITU CHA KUJIFUNZA KUTOKA KWENYE NYASI


 

Jipatie nakala hii kwa 5,000 tu. Tuwasiliane 0755848391

Habari ya asubuhi rafiki yangu!

Siku ya leo napenda tujifunze kutoka kwa nyasi! Ndio nyasi kama nyasi😀.

Nyasi huwa zinaonewa sana. Mara utakuta zimechomwa moto. Siku nyingine zimekanyagwa.

Wakati mwingine zimelimwa.

Au kufyekwa.

Ila mara zote hizo huwa zinaota tena. Ukizichoma moto inakuwa kama umeziita, zinaota kwa spidi na kwa wingi.

Hivyo hivyo ukifyeka, ukizipalilia au kuzikanyaga.

Nyasi zinashangaza, hazikati tamaa hata zikifanyiwa ukatili. Badala yake ndio inakuwa kama unaziita zaidi. 

Kitu hiki pia unapaswa kukitumia wewe maishani mwako. Kama kuna kitu unafanya, kikashindwa usikate tamaa na kurudi nyuma, badala yake iwe kama vile ndio umeitwa. 

Ukianza kuuza bidhaa watu wakaikataa, usikate tamaa, ndio kwanza kumekucha.

Ukipiga simu kuongea na mtu juu ya jambo fulani akawa hajakubali, fahamu kuna wengine watakukubalia, usikate tamaa endelea kuwapigia wengine.

JIFUNZE ZAIDI HAPA: Somo Kubwa La Kujifunza Kutoka Kwa Tony Robins

Ujumbe muhimu ninaotaka uondoke nao leo ni kutokata tamaa, maana siku zote NYUMA YA USHINDI, Kuna kushindwa, kushindwa, kushindwa.

Kupata kitabu cha NYUMA YA USHINDI Kwa 5,000/- tu. Nitumie ujumbe kwa WhatsApp sasa.

Umekuwa nami rafiki yako,

Godius Rweyongeza (Songambele)

Morogoro-Tz


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X