Siku ya leo nina booonge la stori!!
Ngoja nicheke kwanza๐๐. Na wewe unaweza kucheka pia๐๐.
Ee bwana ee, siku hiyo bhana jamaa ndio alikuwa kwenye msiba wa kaka yake, akiwa na majonzi ya kumpoteza mpendwa wake. Hiyo ilikuwa ni miaka 1880, kabla ya simu janja kama hii ninayoitumia leo kukuandikia andiko hili. Lakini pia kipindi hicho facebook hata ilikuwa haifikiriki. Kama mtu kipindi hicho angezungumzia masuala ya twitter au instagram ni wazi Kuwa angeonekana kichaa, au la basi hiyo ingekuwa ni hadithi ya kufikirika (fiction-story).
Kwa hiyo njia pekee, ya uhakika na haraka๐ ya kupata habari ilikuwa ni gazeti.
Jamaa siku hiyo alinunua gazeti, akaanza kulifunua mdogomdogo.
Huku akiwa na hamu ya kupata habari mpya na za motomoto.
Ee bwama ee! Unajua nini? Kwenye kichwa cha mbele , palikuwa pameandikwa, muuza kifo, sasa kifo kimemkuta!
Ndani gazeti liliendelea kuandika kuwa mtu aliyegundua njia ya kuua watu wengi kwa wakati mmoja sasa naye ameaga dunia.
Hicho kilikuwa ni kipindi kabla ya bomu la nyuklia na haidrojeni. Wala kipindi hicho hakuna mtu ambaye alikuwa anafikiria eti kungetokea vita wakatumia ndege.
Moja ya kifaa cha kivita kilichokuwa kinaogopwa sana ilikuwa ni baruti. Na aliyekuwa amegundua kifaa hicho ni mwanasayansi Alfred Nobel.
Sasa siku hiyo alikuwa kwenye msiba wa kaka yake anasoma Gazeti lililokuwa limemuandika yeye kama muuza kifo, na gazeti hilo lilitangaza Kuwa sasa alikuwa ameaga dunia.
Kumbe jamaa mweyewe bado alikuwa hai, ila kaka yake ndio alikuwa ameaga dunia. Gazeti lilichanganya kifo cha kaka yake na yeye mwenyewe.
Na chanzo cha gazeti kuchanganya ni kwamba, ilikuwa ndugu hao wasafiri pamoja, ila Alfred akawa amehairisha hiyo safari. Kaka yake aliendelea na baadaye akapata ajali na kuaga dunia. Sasa gazeti likadhania na Nobel alikuwa kwenye hiyo ajali.
Kusoma ile habari, Nobel akabaki kujiuliza, hivi kumbe nikifa ndivyo magazeti yataniandika? Daah! ikabidi sasa atafute namna nzuri itakayomfanya akumbukwe vizuri, na sio kukumbukwa kama muuza kifo kama gazeti lilivyokuwa limeandika.
Hivyo akawa ameanzisha tuzo za Nobel. Tuzo ambazo leo hii ni maarufu na zinaheshimika sana.
Ninachotaka ufahamu leo ni kwa jinsi gani unaweza kuacha alama hapa duniani. Kuna vitu vitano ambavyo unaweza kufanya ili kuacha alama ya kudumu
1. Andika kitabu, kitaishi miaka mingi hata baada ya wewe Kuwa umeaga dunia.
2. Panda miti (itaishi miaka mingi pia).
3. Sanifu majengo (majengo yana uwezo pia kuishi miaka mingi baada ya kifo)
4. Anzisha/gundua Kitu ambacho kinagusa maisha ya watu. Mfano Steve jobs tutaendelea kumkumbuka kwa miaka mingi kwa sababu tu ya smartphones na kompyuta.
5. Anzisha kampuni iyakayoishi hata baadae ya kifo chako. Mfano mzuri ni kampuni ya cocacola, Ford motors na GM. waanzilishi wake walishaaga dunia, ila kampuni hizi bado zinaishi.
Kwa hiyo hizo ndizo njia nne ambazo unaweza kutumia wewe hapo, kufanya vitu ambavyo vitaacha alama ya kudumu hapa duniani. Walau kati ya hivyo vitu vinne huwezi kukosa kimoja ambacho utakifanikisha.
Naomba nimalizie kwa maneno ya Robin Sharma ambaye ni mwandishi wa vitabu anayesema, ulipozaliwa watu walicheka wakati wewe ukilia unapaswa kuishi maisha kiasi kwamba ukifa ucheke wakati watu wakilia.
Makala hii imeandaliwa na Godius Rweyongeza
0755848391
MOROGORO-Tz
www.songambeleblog.blogspot.com
Jipatie vitabu vyangu kupitia mtandao wa GETVALUE kwa kubonyeza hapa
https://www.getvalue.co/home/seller_collection/393
Mtandao huu wa GETVALUE unakuwezesha wewe kupata nakala laini.
Ili kupata kitabu changu chagua kitabu kimojawapo mfano; chagua KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI.
baada ya hapo bonyeza sehemu iliyoandikwa BUY NOW
Itakupelela sehemu ya malipo.
Utakamilisha malipo.
Kisha baada ya hapo utapakua app ya GETVALUE na kuiweka kwenye simu yako. Kama unayo basi utafungua kitabu hicho kweye app hiyo na kuanza kukisoma.
Pata vitabu vyangu sasa.๐๐