Mambo Matatu Ya Kujifunza Kutoka Kwa Taifa La Israel


 

 

Moja ya taifa ambalo limepiga hatua kiuchumi ni taifa la Israel. Taifa hili sio kwamba lina rasilimali kubwa sana ukilinganisha na mataifa mengine. HAPANA.

Kuna kipindi taifa hili hili lilikuwa na uchumi wa chini sana. sasa hapa kuna vitu ambavyo vinalifanya taifa hili hapa kuendelea na kuzidi kupanuka.

1. wananchi wake kuthubutu. Wanathubutu na kuchukua hatua za kufanya vitu hata vile ambavyo wakati mwingine unaweza kuona kuwa ni vya hatari. Ila mwisho wa siku unakuta kwamba vitu hivyo vinafanyika kwa ubora na hatimaye kuwalipa wale watu. na hata pale wanaposhindwa, sio kwamba huo  unakuwa mwisho wao kufanyia kazi kile kitu, bali wanajifunza, wanachukua somo na kuendelea mbele bila kuacha. Kwenye hili hapa usemi wa Thomas Edison ndio wanatumia. Yaani kuwa hawajafeli mara elfu kumi, badala yake wamejifunza mbinu elfu kumi za kufanya kitu kifanye kazi. ndio maana, utakuta assilimia kubwa ya watu wanaopata tuzo za Nobel ni waebrania. Lakini pia utakuta kuwa hata gunduzi kadha wa kadha kwenye teknolojia, kilimo na maeneo mengine ni za Kiebrania.

 

2. kitu cha pili ni kuwa kila mtu anafahamu kuwa jukumu la kujenga uchumi wa taifa linaanza na mtu binafsi. Kama kila mtu akiinua uchumi wake ni wazi kuwa uchumi wa taifa utainuka. La sivyo zitakuwa ni kelele za mara kwa mara za watu kuwa uchumi umepanda ila fedha hatuzioni. Kwa hiyo kila mtu anachofanya ni kuhakikisha kwamba yeye mwenywe bila kumtegemea mtu mwingine au serikali yake anajenga uchumi wake binafsi na kuukuza.

 

3. Tatu ni wanachi kujenga utaratibu wa kuweka akiba. Hii dhana ambayo inaanzia kwenye dini yao ya kiyahudi na kuja kwenye maisha yao ya kila siku. Hivyo, mtoto tangu akiwa mchanga anafundishwa kuwa kuna fungu la kumi la kumtolea Mungu. Lakini pia anafundishwa kuwa kuna fungu la kumi la akiba. Kwa hiyo kwa kila fedha anayopokea anapaswa kuhakikisha ametoa fungu la Mungu na fungu lake la akiba.

Utaratibu huu ni mzuri maana ukiangalia karibia mikononi mwa kila mtu huwa kuna fedha nyingi zinapita tangu anapozaliwa. Ila sasa linapokuja suala zima la kazi ya hizo fedha ndilo linatofautiana. Kuna watu tangu wamezaliwa wameshapokea mamilioni ya fedha ila mfukoni unakuta kuwa hawana hata senti moja, wala hawajawekeza sehemu yoyote. Kwa kuliona hilo hapo nimeona nikuandalie kitabu cha MAAJABU YA KUWEKA AKIBA.

Unaweza kujipatia nakala yako siku ya leo kwa na kujifunza maajabu ya kuweka akiba kwa kubonyeza HAPA

https://www.getvalue.co/home/product_details/maajabu_ya_kuweka_akiba

 

Kwa hiyo rafiki yangu hayo ndiyo mambo matatu ambayo unaweza kujifunza kutoka kwenye taifa la lsrael na kuyafanyia kazi kwenye maisha yako ya kila siku ili kupata matokeo makubwa.

Nakutakia kazi njema katika kufanyia kazi haya yote uliyojifunza HAPA.

 

Umekuwa name rafiki yako,

Godius Rweyongeza

0755848391

Morogoro-Tz


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X