Ni mpaka pale unapofanya kitu kinapowezekana


Mara nyingi vitu vingi huwa vinaonekana haviwezekani. ila ukiamua kwa dhati kuvifanyia kazi lazima tu vitawezekana.

Kwa vile vitu ambavyo wewe umekuwa unaona haviwezekani, ebu amua kuwa ndani ya wiki hii ambayo tumeanza kuwa unaenda kuvifanya. na kweli vifanye bila kukosa.

Mwisho wa siku utajikuta kwamba umeweza kutimiza vile ambavyo watu walikuwa wanasema haiwezekani, au hata vile ulivyokuwa wewe mwenyewe unaona kwamba haviwezekani.

Kuna nyakati unapaswa kwenda kinyume na imani za wengi, au hata imani ulizo nazo wewe mwenyewe juu yako. na imani hizi ni pamoja na hivyo vitu ambavyo kwa sasa unaamini huwezi,

Chagua kitu kimoja ambacho unaona kuwa hakiwezekani na kifanye hicho. kila la kheri.

Umekuwa nami, Godius Rweyongeza

Jiunge nami youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Pata vitabu vyangu kwa KUBONYEZA HAPA

Kupata makala maalumu kwa watu maalumu basi BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X