SITAKI UNAFIKI; Mambo Saba Ya Kufanya Unapokuwa Na Ndoto Kubwa


 

Jamii yetu inafurahisha sana, Kuna baadhi ya vitu ambavyo ukisema au kufanya, basi utaonekana mwema na mtu anayefaa. Ila kuna vitu ambavyo ukisema au kufanya basi utaonekana mnafiki, asiyefaa na mwenye tamaa.

Waambie watu kuwa unapenda kuajiriwa basi watakufurahia kwelikweli. Ila waambie hutaki, wakati wanaona kabisa vyeti vyako viko vizuri kwa asilimia mia, watakimbilia kusema umelogwa, akili zimeruka, ukisoma sana unapoteza mwelekeo n.k 

Waambie watu kuwa unataka kununua baiskeli, hakuna hata atakayekushangaa. Wala hakuna atakayeaema FIKIRI KWA UKUBWA.

Ila waambie watu kuwa utanunua ndege binafsi, watakwambia kila aina ya maneno. Wapo watakaosema  haiwezekani, wengine watasema haijawahi kufanyika,  wengine watakuuliza ya kuchora au? Na wengine watasema kwani siku hizi zinaokotwa!? Sasa Mimi SITAKI UNAFIKI.

Hapa ninaenda kukueleza mambo muhimu ya kufanya unapokuwa na ndoto kubwa.

1. Jikumbushe ndoto yako mara kwa mara.

2. Ungana na watu wananaoamini kwenye ndoto yako.

3. Usikae karibu na wakatisha tamaa.

Watakupunguzia motisha yako ya kufanya makubwa.

4. Ifanyie kazi ndoto yako kila siku.

5. Soma vitabu vinavyoendana na ndoto yako vitabu vya hamasa. Anza na KUTOKA SIFURI MPAKA KIKELENI au JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO tuwasiliane leo leo kwa 0755848391

6. Jifunze kutoka kwa watu waliokuwa na ndoto kama yako, wakaifanyia kazi na kuifanikisha.

7. Kama unaanzia chini jifunze kwa watu walioanzia chini mpaka wakaweza kufikia kwenye kilele cha mafanikio.

8. Jipe muda wa kuifikia hiyo ndoto yako. Vitu vizuri vinahitaji muda. Huwezi kukurupuka leo ukiwa unahitaji kutimiza ndoto kubwa, ikatimia siku hiyohiyo.

Nakubaliana na Jack Ma anayesema, 

vitu vingine havihitaji haraka, huwezi kuwapa wanawake tisa mimba ndani ya mwezi mmoja, huku ukitegemea kupata mtoto ndani ya mwezi huohuo.”

Hayo ndiyo mambo nane ya kufanya unapokuwa na ndoto kubwa rafiki yangu. Kila la kheri.

Sasa jipatie nakala ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KIKELENI kutoka kwangu. Cha kufanya nipigie au nitumie ujumbe kwenda 0755848391.

Gharama ya kitabu hiki ni 10,000/- tu

 Utakipata popote ulipo nchini.

Vitabu vyangu vingine hivi hapa

https://www.getvalue.co/bhome/seller_collection/393

Jiunge nami YouTube kwa kubonyeza hapa

Kupata makala maalumu kwa watu maalumu basi BONYEZA HAPA


One response to “SITAKI UNAFIKI; Mambo Saba Ya Kufanya Unapokuwa Na Ndoto Kubwa”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X