TOFAUTI KATI YA BLOGU NA TOVUTI


 

 Moja ya swali ambalo watu wanapenda kuuliza ni tofauti kati ya blogu na tovuti.

Siku ya leo nimeona nikueleze hizi tofauti ili na wewe uweze kuzifahamu.

Blogu ni aina ya tovuti ambayo machapisho yake hujipanga kwa mangilio, huku yale yaliyowekwa kwa tarehe za karibuni yakionekana juu zaidi ukilinganisha ya yale ambayo yaliwekwa tarehe za siku za nyuma.

 

Mwanzoni blogu zilikuwa zinatumika kama diary za mtandaoni, ambapo watu walikuwa wanaweka vitu mbalimbali kwa siku husika. Lakini kadiri siku zilivyoendelea zikawa zimeanza kuwa chanzo cha kipato kwa baadhi ya watu na hivyo kuzidi kupata umaarufu zaidi.

 

Kwa kawaida blogu huendeshwa na watu binafsi au kikundi cha watu na huwa hazina mbwembwe nyingi kwenye kuendesha. Yaani, hazihitaji utaalamu wowote kwenye kuendesha. Mtu yeyote ambaye anamiliki barua pepe, anakuwa na uwezo wa kuedesha blogu bila shida yoyote

 

Tovuti yenyewe kwa upande wake sio lazima ioneshe kazi zilizowekwa kwa mpangilio maalumu kama ilivyo kwa blogu. Tovuti hazibadilishwi kilichomo mara kwa mara. Lakini pia tovuti zinahitaji utaalamu kidogo wa kuendesha kulinganisha na blogu.

 

JE, KATI YA BLOGU NA TOVUTI KIPI NI BORA ZAIDI?

Mara nyingi tovuti huwa zinakuwa na taarifa muhimu kuhusiana na biashara au taasisi. Kwa mfano mawasiliano ya kampuni, maelezo mafupu kuhusu taasisi au kampuni, shuhuda za watu, eneo kampuni au biashara ilipo, maswali yanayoulizwa mara kwa mara, n.k.

Unaweza kuwa tovuti lakinilpia na blogu. Tovuti haibadiliki mara kwa mara, ila kwenye blogu  unakuwa unaweka vitumbalimbali kama kuelimisha watu wake kuhusu bidhaa au vitu mbalimbali vinavyopatikana kwenye kampuni, biashara au taasisi husika.

 

Ndio maana ukitembelea tovuti za baadhi ya taasisi utakuta kuna kipengele cha visit our blog.  Yaani, tembelea blogu yetu. Maana huko ndiko huwa wanaweka vitu mbalimbali vya kuelimisha.

 

Tovuti pia huwa zina gharama kubwa kwenye kuanzisha kulinganisha na blogu. Kwa hiyo kama unaanza, unaweza kuanza kwa kutengeneza blogu, kama utakuwa na mpango wa kuibadili kwenda kwenye tovuti unaweza kufanya hivyo baadae kulingana na unavyokua.

 

Karibu nikutengenezee blogu yako leo hii. Tuwasiliane kwa 0755848391 

Imeandailwa na GODIUS RWEYONGEZA

Tuwasiliane kwa 0755848391

 

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X