Umuhimu Wa Kuw Na Misingi Unayosimamia Maishani


 

Ni muhimu sana kwenye maisha yako kuwa na misimamo na kuhakikisha kwamba unaisimamia, ikitokea kwamba umevunja msingi mmoja, utajikuta kwamba unavunja kila msingi ambao umejiwekea kwenye maisha na hivyo kuanza kuishi maisha ambayo hayana maana.

Jijengee misingi sahihi, ifuate na iishi hiyo misingi bila kujali kwamba unapitia katikahali gani. kuna vitu vidogo unaweza kuona ni vya kawaida ila kumbe madhara yake yakaja kuwa makubwa kwenye maisha yako. Ebu kwa mfano tu tuseme kwamba moja ya msingi wako ni kutokutoa rushwa maishani mwako.

Lakini ikitokea siku moja ukashawishika kuitoa, utakuwa umeuvunja huo msingi na utajikuta kwamba siku nyingine unauvunja huo msingi. Na sio hilo tu, utaanza kuona kwamba ulipovunja huo msingi hakuna kitu chochote kilichotokea, hivyo, utajikuta ukivunja na misingi mingine. Kitu hiki kitakufanya uwe mtu ambaye anaishi maisha ya hovyo, badala ya kuishi maisha yaliyopangiliwa na maisha ambayo huna chochote unachosimamia.

 

Kwa hiyo ni muhimu sana kufahamu kuwa unapaswa kuwa na misingi sahihi maishani mwako. Isimamie hiyo misingi yako bila kutetereka.

Kila la kheri.

 

Godius Rweyongeza

0755848391

Hakikisha umesubscribe kwenye youtube channel yangu kwa ajili ya mafunzo ambayo ninakuwekea huko kila siku. BONYEZA HAPA SASA HIVI.

Kupata vitabu vyangu basi BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X