FANYIA KAZI UNACHOJUA


 

Ujue unaweza kuwa unajua mambo mengi. Ukawa unajua hatua muhimu unazopaswa kuchukua, Ila kama hutachukua na kufanyia kazi kile unachojua, basi ni wazi kuwa usitegemee kupata matokeo yanayoendana na maarifa uliyonayo.

Kitu kikubwa unachoweza kufanya ni kuweka kwenye MATENDO ulichojifunza.

Ukijifunza kuhusu kuweka AKIBA, weka.

Ukijifunza kuhusu kulala  kuamka mapema fanya hivyo. Hakuna njia nyingine ya mkato ya wewe kupata matokeo bila kuweka kazi.

Napenda nimalizie kwa kusema kuwa unaweza kumwonesha tembo maji ila huwezi kumlazimiaha kuyanywa. Unapojifunza au kusoma vitabu, ni kama unaonoshwa maji. Jukumu lako ni kuyanywa. Hakuna mtu anaweza kukufanyia wewe kazi hiyo.

Hakuna mtu anaweza kukusaidia wewe kupiga push-up zako

Hakuna mtu anaweza kufanya mazoezi kwa niaba yako.

TUKUTANE KWENYE JUKWAA LA WANAMAFANIKIO

Godius Rweyongeza

Morogoro-Tz

0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X