KABLA HUJALAMIKIA MAMBO 100 AMBAYO HAUNA SHUKURU KWA MAMBO 10 ULIYONAYO


Unaweza kuwa mtu mzuri kwa kulalamika kwa vile vitu ambavyo hauna.

Unalalamika hauna ajira. 

Unalalamika watu wako wa karibu hawakujali. Unalamila hauna konekisheni.

Lakini kabla ya kulalamikia hivyo vitu vyote, umeshakaa chini na kujiuliza ni vitu gani vichache ulivyonavyo? Ni vitu gani vichache unaweza kushukuru kwa kuwa navyo?

Ujue leo hii unapumua. Kuna watu walitamani kuwa wanapumua ila hawajaweza. 

Unalalamikia hauna ajira Ila walau umesoma, kuna watu wanatamani wangekuwa walau wamesoma kama wewe.

Siku ya leo itapendeza kama utakaa chini na kuandika orodha ya vitu ulivyonavyo. Vitu ambavyo unashukuru kuwa navyo. Inaweza kuwa Ni kipaji chako, elimu yako, ujuzi wako, mahusiano yako n.k. SHUKURU KWA kuwa na hivi vitu.

Ni rahisi kupata kitu unapokuwa na kitu kuliko unapokuwa hauna.

Kwa mfano, ni rahisi kupata kazi ukiwa na kazi kuliko pale unapokuwa hauna kazi.

Hivyo hivyo kwako, badala ya kulalamika kwa vitu ambavyo hauna, basi shukuru kwa vile ulivyonavyo maana siku zote Ni rahisi kupata kitu unapokuwa na kitu kuliko pale unapokuwa hauna! Ukishukuru kwa kile ulichonacho inaonesha kuwa una kitu. Hivyo, utaweza kupata kingine maana tayari una kitu.

Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

 

Kutengenezewa blogu yako kitalaamu tuwasiliane kwa 0755848391

kila la kheri


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X