Kauli Saba Unazopaswa Kuziondoa Kwenye Kamusi Ya Maongezi Yako


https://www.getvalue.co/home/product_details/kutoka_sifuri_mpaka_kileleni

 

 

Maneno huumba. Ni usemi mfupi wa wahenga ila wenye maana kubwa sana. ni ukweli kuwa maneno yana uwezo wa kuumba kitu chochote. Ukitaka maneno yakuumbie kitu kizuri, basi unaongea maneno chanya. Ukitaka maneno yakuumbie kitu kibaya basi unaongea unaongea maneno hasi. Ni hivyo tu. Sasa siku ya leo nimeona nikuletee kauli tano ambazo unapaswa kuziondoa kwenye kamusi ya maongezi yako. La sivyo kauli hizi hapa zinaenda kukuangusha chini na kukufanya uendelee kupata matokeo mabaya. Kauli zenyewe ni

 

1. NIPO TU NAHANGAIKA

Hii ni kauli ambayo watu wengi wanapenda kuitumia. Kadiri unavyokuwa unasema kwamba unahangaika ndivyo unaendelea kupata kuhangaika zaidi. maana wewe unachojua kwenye kamusi yako ni kuhangaika. Unapata unachosema. Kama unasema unahangaika, basi unastahli kuendelea kuhangaika zaidi.

 

2. MAISHA NI MAGUMU au HALI NI MBAYA au MAMBO NI MAGUMU

Kama ambavyo tayari nimeshaeleza hapo awali. Unapata unachosema. Ukisema maisha ni magumu, utaendelea kupata ugumu zaidi maana wewe unachopenda kupata ni kile unachosema.

3. NINAYUMBA KAMA DELA

Ukisema unayumba, utaendelea kuyumba mpaka siku utakapoamua kusema kwamba sasa wewe u imara.

 

4. NINAJARIBU

Kujaribu ni tofauti na kufanya. Kwa hiyo ukisema kwamba ninajaribu inakuwa inaashiria kwamba hujajitoa kabisa kufanya hicho kitu kwa uhakika. Ila ukisema kwamba nimeamua kufanya hiki kitu au nimedhamiria kufanya hiki kitu, maana yake unakuwa umejitoa kabisa. kwa hiyo kuanzia leo hii epuka kusema kwamba ninajaribu. Kumbuka ni au unafanya au hufanyi, ila hakuna kitu cha katikati hapa kinachoitwa kujaribu.

Kuanzia leo hii anza kufanya au la amua kutofanya kabisa.

 

 5. HAIWEZEKANI

Hii ni kauli nyingine ambayo unapaswa kuiondoa kwenye kamusi ya maongezi yako. Ukisema kwamba haiwezekani, unakuwa unaondoa uwezekano wa kufikiri nje ya boksi na kuona jinsi kitu hicho kinavyoweza kufanyika na kuja katika uhalisia.

 

6. SIWEZI KUPATA HIKI KITU

Ukisema kwamba huwezi kupata kitu fulani, unakuwa unafunga sehemu ya akili yako ambayo huwa inafikiria na kukuletea mbinu za kupata kitu chochote unachohitaji maishani mwako. Kwa hiyo, badala ya kusema kwamba; huwezi kupata kitu fulani, jiulize ni kwa jinsi gani ninaweza kupata kitu hiki? Akili yako itafunguaka na kukuletea njia ambazo hata mwanzoni ulikuwa hujafikiria, zitakazokuwezesha kupata hicho kitu.

 

7. SIKU HIZI FEDHA IMEKUWA NGUMU

Ukisema fedha imekuwa ngumu, ni wazi kuwa utaendelea kupata ugumu zaidi.  badala yake jisemee maneno chanya kuhusu fedha na ambayo yataivuta fedha kwako.

Ikumbukwe kwamba siku zote unavuna ulichopanda. Hivyo, ukitaka kubadili kile unachopata lazima uwe tayari kupanda kitu cha tofauti. Hata kamautakuwa unapitia kwenye changamoto kubwa, kamwe usithubutu kuongea hayo maneno. badala yake jinenee maneno chanya. Sema kwamba;

·         maisha ni mazuri,

·          nimezaliwa kushinda,

·          mimi ni sumaku ya fedha,

·         fedha zinanipenda na zinakuja kwangu.

·         Nina afya njema,

·         Nina utajiri na busara za kutosha,

Asili ya dunia ilivyo ni kwamba kile unachosema kwamba unacho, ndio unakipata zaidi. kwa hiyo, ukiendea kusema hayo maneno utaenelea kupata zaidi kile unachosema. Ila ukiyabadili na kuelekeza nguvu kwenye vitu vingine ni wazi kuwa utapata hivyo vitu.

Kujifunza zaidi kuhusu nguvu ya kauli zako unazotoa, nashauri ujipatie nakala ya kitabu cha KUTOKAA SIFURI MPAKA KILELENI, kwenye kitabu hiki sura ya nne imeeleza kwa kina juu ya kauli na jinsi ambavyo zinaweza kukufanya ufanikiwe maishani. unaweza kupata nakala laini kwa kubonyeza HAPA au bonyeza picha iliyowekwa mwanzoni mwa makala hii.

Nakala ngumu utaipata kwa kuwasiliana nami kwa 0755848391

Kila la kheri

Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

 Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391

Kutengenezewa blogu yako kitalaamu tuwasiliane kwa 0755848391

kila la kheri


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X