Kuhusu Kufanya Maamuzi


 Kuna wakati unajikuta njia panda ukiwa unatakiwa kutoa maamuzi. Lakini unashindwa ufanye nini au usifanye nini. Kitu muhimu kufahamu ni kuwa unapaswa kufanya maamuzi. Kufanya maamuzi ni bora kuliko kutokuchukua hatua kabisa.

Ukifanya maamuzi ukakuta hayakuwa sahihi, utajifunza na kuendelea mbele.

Kama yalikuwa maamuzi sahihi ni wazi kuwa utanufaika. Lakini usipochukua hatua na kubaki kwenye hiyo njia panda hautapata chochote.

Kwa hiyo Leo hii kachukue hatua na ufanye kitu.

Kila la kheri

Godius Rweyongeza

Morogoro-T

0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X