Nafasi za kuingia darasani kujifunza uandishi zinaelekea kuisha. Changamka sasa hivi, usije kupitwa na fursa hii hapa


 

Juzi nilitangaza nafasi kwa ajili ya watu ambao wangependa kujifunza uandishi. Watu hawa wanaenda kuhudhuria darasa maalumu la uandishi ambalo litaendeshwa kwa siku 33 mfululizo. Kwenye darasa hili hapa tunaenda kujifunza mbinu zote za kiuandishi ambazo zitakufanya wewe uweze kuwa mwandishi mbobevu.

Kama kuna maswali ambayo umekuwa unajiuliza kuhusu uandishi, yote yatajibiwa.

Kwa mfano kama unajiuliza, nawezaje kuwa mwandishi. Naanza anzaje hasa? Kwenye darasa hili hapa utaoneshwa njia ya kuanzia. Kiufupi ni kwamba hata kama hujawahi kuandika, darasa hili hapa linaenda kukupa mbinu za kukusaidia wewe kuandika. Njoo nawe utaona.

 

Kama unajiuliza, hivi waandishi huwa wanapata wapi vitu vya kuandikia, ninachoweza kukwambia kwa sasa hivi ni kwamba kuwa na subira bado kitambo kidogo tu. tarehe 20 ya mwezi huu wa kumi sio mbali. Swali lako litajibiwa na dukuduku lolote utakalokuwa nalo, litaondolewa.

 

Kiukweli darasa hili hapa linaenda kuwa ni la kipekee sana. ila sasa cha kushangaza ni kwamba usipochangamka, basi hili darasa unaenda kulikosa. Ndio, utalikosa hivi hivi. Hii ni kutokana na ukweli kuwa nafasi zimebaki mbili tu mpaka sasa hivi. Usipochangamka leo hii, yaani sasa hivi basi darasa hili utalikosa.

 

Idadi wa watu watakaohudhuria darasa hili maalumu ni tano tu. hakikisha unajiingiza kwenye orodha ya watu hawa wachache watakaohudhuria darasa hili leo hii

Kitu pekee ambacho unaweza kufanya sasa hivi ni kusoma maelezo haya na kisha kuchukua hatua

SOMA ZAIDI; NINAHITAJI WATU WATANO, NAMI NITAWAFANYA KUWA WAANDISHI WABOBEVU NDANI YA SIKU 33 

Kila la kheri.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X