USIJILINGANISHE NA WATU WENGINE


 Kama kuna dhambi kubwa ambayo unaweza kufanya ni dhambi ya kujilinganisha na watu wengine. 

Ujue huwezi kufanya kitu original kama wewe ni mtu wa kujilinganisha na watu wengine.

 Maana wewe muda wote tu, utakuwa unaangalia nani, amefanya nini? Na nani hajafanya nini? 

Na wewe utakuwa unaiga walivyofanya ili uweze kuendana nao! Kila wakifanya kitu fulani na wewe unakimbilia kufanya hicho kitu. Kwa jinsi hiyo huwezi kuwa original! Na Wala huwezi kufanya kitu kikaeleweka kuwa Ni chako.

Kitu muhimu kuzingatia ni kuwa unahitaji kuamua kufanya kitu chako hata kama machoni pa watu kitaonekana ni cha kijinga.. Huyo mwingine naye mwache afanye Cha kwake. 

Kama itatokea unapaswa kujilinganisha, basi jilinganishe na wewe wa jana pamoja na wewe wa leo.

Wewe mwaka Jana na wewe wa mwaka huu.

Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

 Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391

Kutengenezewa blogu yako kitalaamu tuwasiliane kwa 0755848391

kila la kheri


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X