Kama kuna kitu muhimu ambacho unapaswa kuwa nacho ili ufanikiwe zaidi basi ni malengo. Ukikutana na mtu mwenye malengo Basi unapata picha halisi ya mtu atakayefanya makubwa maishani. Ila ambaye hana malengo ni wazi kuwa atakuwa anayumba kama bendera.
Wakati mwingine unaweza kuwa na malengo Ila ukawa kama ambaye hana malengo. Na vifuatavyo Ni vitu vinavyoweza kudhihirisha hilo.
1.Kama una malengo ambayo hujayaandika, basi ujue kuwa itakuwa vigumu kwako kuyatimiza.
2.kama una malengo ambayo hayana ukomo wa muda, ujue itakuwa vigumu kuyatimiza.
3. Kama una malengo ambayo umeyaweka muda mrefu ila hujawahi kuchukua hatua kuyafanyia kazi ujue hutaweza kuyatimiza.
4. Kama una malengo ambayo huyasomi na kuchukua hatua kila siku, ujue itakuwa vigumu kwako kuyatimiza
5. Kama malengo yako ni kufanya kila kitu ujue pia hutaweza kufikia chochote
Kwa hiyo unapaswa kuepuka malengo ya aina hiyo kwa kuhakikisha malengo yako umeyaandika kwenye daftari na umeyawekea ukomo, unayafanyia kazi kila siku hata kama ni kwa hatua ndogo.
Kila la kheri