Vitu Vitano Unavyopaswa Kufanya Kama Umeajiriwa


 

Hapo zamani za kale mfumo wa ajira haukuwepo kabisa. Hata hivyo, zilipoanza zama za viwanda, ndipo na mfumo rasmi wa elimu ukawekwa ili kuzalsisha watu wa aina fulani waliokuw wanahitajika kwenye viwanda lakini wakati huohuo mfumo wa ajira nao ukazaliwa. Kipindi hicho, watu walikuwa wanaandaliwa shuleni ili kukidhi mahitaji yaliyokuwepo kwenye viwanda. na kutokana na ukweli kwamba watu hawakuwa wengi kwenye soko la ajira basi uhitaji wa watu ukawa ni mkubwa. Kwa hiyo, ikawa ni kwamba ukiandaliwa na mfumo wa elimu na kuingia kwenye soko la ajira basi ajira ni nje nje.

Kilichofuata kila mtu akaanza kukimbilia kwenye mfumo wa elimu ili afunzwe kukidhi mahitaji ya kwenda kufanya kazi viwandani. Baada ya muda mfupi kila mtu alilkuwa ameanini kwamba ajira ndio kila kitu. Mfumo wa ajira hauna miaka mingi tangu umeanza ukilinganisha na umri wa binadamu kwenye hii dunia. Wakati binadamu amekuwepo kwenye hi dunia kwa zaidi ya miaka milioni 2. Mfumo wa ajira hauna hata zaidi ya miaka 300 tangu umeanziswa, ila umetokea kuwa kitu kinachoaminiwa na watu wengi na kimekuwa ni kitu ambacho kimesambaa kwa haraka zaidi karibia kwenye kila kona ya dunia.

Pengine mfumo wa ajira unaweza kuwa umesambaa haraka na kuaminiwa wa na watu wengi zaidi ndani ya muda mfupi kuliko hata dini zilivyosambaa kwa haraka kutoka eneo moja kwenda jingine!

Knachowafanya watu wepende ajira ni uhakika wa mshahara lakini wenngine wana imani kwamba wanaweza kupata mafanikio makubwa wakiwa ndani ya ajira. Hata hivyo ni ukweli kuwa huwezi kupata mafanikio makubwa ukiwa ndani ya ajira ni mpaka pele utakapoamua kutoka nnje ya ajira ndipo unaweza kupata mafanikio kwa kiwango unachotaka wewe. Hiki ni kitu ambacho sikupenda kuwa wa kwanza kukwambia ila sasa inanipasa kusema hivyo,  Sasa hapa kuna vitu vitano ambavyo utapaswa kufanya kama umeajiriwa ili viweze kukusogeza kwenye mafankio makubwa

 


KWANZA NI KUONGEZA JUHUDI ZA KUJIFUNZA

Kama mpaka umefuatilia vizuri kuna vitu viwili vikubwa ambavyo tumeviona. Kwanza ni mfumo wa elimu ambao umeanzishwa ili kuzalisha watu wa aina fulani wanaohitajika kwenye soko mfumo wa pili ambao ni mfumo wa ajira. Mfumo wa elimu unazalisha watu wa aina moja (photocopy). Ukiingia kwenye mfumo wa elimu utafundishwa sawa na mwenzako na profesa ni yuleyule labda tu kama utaamua kujitofautisha wewe mwenyewe. sasa kama hautajitofautisha wewe mwenywee, hii ndio kusema kwamba wewe hautakuwa na tofauti na wengine. Kile ambacho utakuwa unafanya wewe, kuna mwingine anaweza kukifanya maana nyote mmezalishwa na mfumo uleule. Hii ndio maana unahitaji kuwa unajifunza na kuongeza maarifa ya kutosha. Kwa kuwa watu wengi huwa hawapendi kuongeza maarifa hasa baada ya kuwa wamehitimu chuo, hiiitakuwa ni nafasi yako wewe kujitofautisha na kuwa mtu wa kipekee.

 

Kitu kingine ni kwamba ukipata maarifa ya tofauti ambayo wengine hawakufundishwa, utakuwa na uwezo wakufanya tofauti na hivyo kitu kitakuongezea thamani kwenye ajira yako. Kwa hiyo kama kuna kitu muhimu sana ambacho unapaswa kufanya kama umeajiriwa, basi ni KUONGEZA JUHUDI KWENYE KUJIFUNZA.

 

 

PILI, NI KUJENGA TABIA YA KUWEKA AKIBA

Kama uko kwenye ajira kuna mojawapo ya kitu kati ya hivi kitakutokea. Kustaafu, kuacha kazi kwa hiari, kufukuzwa kazi (kuachiswa kazi). kwa vyovyote vile kuna siku kitu kimojawapo kati ya hivyo kitatokea. Sasa si jambo la busara ukose kujipanga kwa ajili ya kesho yako. Na moja ya njia ya kujipnga kwa ajili ya kesho yako ni kuhakikisha kwamba unaanza kuweka akiba kwa ajili ya kesho. Sasa hivi mambo yakiwa ni mazuri ili huwezi kuipangilia kesho yako. Hivyo, jipange kwa ajili ya kesho.

 

TATU, JENGA TABIA MPYA

Mara zote mshahara wa mwajiriwa huwa hautoshi. Akiupokea mwishoni mwa mwezi mpaka kufikia mwezi ujao mshahara umeisha. Imefikia hatua umetokea usemi kuwa mishahara huwa haikutani. Na wengine wanafikia hatua ya kuamini kwamba mishahara huwa ina mkosi au fedha ya mshahara huwa haikai. Wengine huwa wanaenda mbali zaidi kwa kusema kwamba fedha ya mtu fulani (mwajiri wake) huwa hata haukai nayo. Wanachonshindwa kutambua ni kwamba  fedha kama fedha haijui hilo. Ila tabia zako wewe mwenyewe ndio zinakupelekea wewe kufanya hivyo. Kwa hiyo, ukibadili tabia zako maana yake unaweza kukaa na fedha zako. mshahara mmoja unaweza kukutana na mshahara mwingine.

Kwa hiyo, kama kuna tabia muhimu sana ambayo unapaswa kuwa nayo kwenye mshahara wako ni tabia ya kuandika kila matumizi unayofanya kila siku. Pia tabia ya kutumia fedha kulingana na kipato chako badala ya kutumia fedha kubwa kuliko mshahara wako, epuka kujikopesha, epuka kutaka kuonekana mtu wa viwango wakati fedha yenyewe wa kujibakiza kwenye viwango hauna, epuke kuhemka unapopokea fedha mpaka kuifanya jamiii nzima ijuie kwamba umepokea mshahara.

 

 NNE, FIKIRI NJE YA AJIRA

Sijawahi kusikia kwamba mwajiriwa fulani ni tajiri. Na hapa ninapoongelea utajiri ninaongelea utajiri haswa sio yale mambo ya kwambna umemiliki gari, sasa ndio umekuwa tajiri. Utajiri wa kuwa na rasilimali na uwekezaji unazokuingizia fedha kiasi kwamba hauna hofu ya pato lako wala suala lolote la fedha. Hili hapa ndilo linapaswa kuwa lengo lako. Lakini huwezi kulifikia lengo hili hapa kama utaendelea kukaa ndani ya ajira. Hivyo, unapaswa kuanza kufikiri nje ya boksi ukiwa ndani ya ajira. Na hatua ya kwanza kabisa ya wewe kuchukua ni kuanzisha bishara nje ya ajira yako. bishara hii unaweza kuwa unaifanyia kazi asubuhi na mapema unapoamka au la unawezakuwa unaifanyia kazi jioni muda unapotoka kazini.

 

Najua utaanza kusema kwamba ninapotoka kazini ninakuwa nimechoka, lla ukweli ni kwamba kama unataka kuuufikia utajiri basi unapaswa kujituma na kufanya vitu kinyume na mazoea. Kama utaendelea kuishi na kufanya vitu kama ambavyo kile mmoja anafanya, ni wazi kuwa utaendelea kupata matokeo ambayo kila mmoja anapata. Na kama utapata matokeo ambayo kila mtu anapata maana yake huwezi kujenga maisha ya tofauti. Utaishia tu kuwa mtu wa kawaida. Tena watu wrngine watadiriki kukuita mnyonge. Ni ujinga kufanya mambo yaleyale huku ukitegemea kupata matokeo ya tofauti.

 

TANO, KUHESHIMU KAZI YAKO YA SASA

Kazi yako (ajira) ya sasa hivi unapaswa kuiheshimu. Maana hii ndio inakufanya uingize mkono kinywani, kwa hiyo, anza kujenga utaratibu wa kuifanya kwa bidii kubwa na kwa kujituma haswa. Hakikisha kwamba unaifanya kwa ubora wa hali ya juu. Kila siku wahi kazini, ukifika kazini weka kazi panapostahili kazi. Achana na sotori zisizo na ulazima, achana na masuala ya kuchati muda wa kazi. acha muda wa kazi uwe wa kazi baadaye huko jioni au muda wa mapumziko utautumia kuchati. Fanya kazi vizuri maana hiyo kazi ndiyo inakuwezesha wewe kuendesha maisha yako ya sasa. ila wakati huhuo usishaukwamba biashara yako ya pembeni nayo itapaswa kuendelea, ili ifikie hatua ambapo utanunua uhuru wako na kutoka kwenye ajira ukiwa hauna shida yoyote.

soma zaidi; Huu Ndio Utumwa Ambao Unapaswa Kuuepuka

Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

 Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391

Kutengenezewa blogu yako kitalaamu tuwasiliane kwa 0755848391

kila la kheri




Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X