Vitu Vitano Usivyojua Kuhusu Biashara Kubwa


Leo mimeyakumbuka maneno ya Jack Ma Mwanzilishi wa kampuni ya Alibaba.  Baada ya kampuni yake kuwa imefanikiwa sana, siku moja alinukuliwa akisema, “unapofanikiwa kila kosa lako linaonekana ni ushujaa, ila ukishindwa kila kosa lako linakuwa takataka”. Kitu hiki ndicho kimenisukuma Leo nukuandikie vitu vitano usivyovijua kuhusu biashara kubwa na kampuni kubwa.

1. Nyuma ya ushindi wa biashara yoyote kubwa, kuna watu wenye maono makubwa, yaliyowezesha kampuni hiyo kufika hapo. Na wewe kama una mpango wa kufanikisha biashara yako, basi hakikisha una maono makubwa.

Tukimchukulia mfano, Jack Ma ambaye nimeanza kwa kutoa nukuu yake hapo juu. Yeye maono makubwa aliyonayo kwa kampuni ya Alibaba ni kuifanya iweze kudumu kwa miaka 102 ijayo.

Sasa wewe maono makubwa ya biashara yako ni yapi?

Kama hauna maono utakwama. Au kwa maneno ya Arnold Schwarzenegger, unaweza kuwa na meli nzuri kuliko zote duniani,ukawa nahodha nzuri kuliko wote. Ila Kama hujui inaelekea wapi,ujue utazunguka huku na huko na kurudi ulipotoka [bila kufanya kitu chochote Cha maana.]

2. Nyuma ya ushindi wa biashara kubwa kuna  watu wanaochapa kazi kuleta matokeo.

Wahenga wanasema ukiona vyaelea, ujue vineundwa. Ukiona kampuni nzuri Basi ujue nyuma yake Kuna watu wanaochapa kazi.

Na wewe Kama unataka kuanzisha biashara yenye mafanikio makubwa, basi usiifanye peke yako.badala yake, shirikiana na watu. Yaani, ajiri.

3. Nyuma ya ushindi wa biashara kubwa Kuna kushindwa, kushindwa, kushindwa.

Kuna wakati biashara hiyo inatengeneza bidhaa ila haiuziki sana. Muda mwingine mapokeo ya bidhaa yanakiwa sio kama ilivyotarajiwa. Lakini wamiliki wa biashara wanajifunza mengi na kisha wanasongambele.

4. Nyuma ya ushindi wa biashara kubwa kuna watu wanafanya kazi masaa 16-18 kila siku kwa siku saba za wiki. Mfano mzuri no Jack Ma. Anaanza kazi saa tatu asubuhi na kumaliza saa tatu usiku kila siku kwa siku saba.

Sasa sijui wewe unafanya kazi kwa muda gani. Ila utapaswa kujirekebisha

5. Nyuma ya ushindi wa biashara kubwa kuna watu wamewekeza rasilimali zao wakati wa kuanzisha biashara mpaka biashara zikafanikiwa.

Kuna vitu wamejinyima ili tu kuwezesha biashara ziende.

Rafiki yangu hivyo ndivyo vitu Vitano Usivyojua Kuhusu Biashara Kubwa.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X