Vitu Vitano Vitakavyokufanya Upate Mafanikio Yasiyo Ya Kawaida


 

https://www.getvalue.co/home/product_details/tatizo_si_rasilimali_zilizopotea

Ni wazi kuwa kila mtu angependa kupata mafanikio makubwa na mafanikio ambayo watu wengine hawawezi kupata. Hata hivyo, si watu wote wanafanya vile vitu ambavyo vinapelekea kwao kupata mafanikio makubwa. ukweli ni kwamba ukifanya vitu ambavyo kila mtu anafanya, utaishia tu kupata matokeo ambayo kila mtu anapata. Ila ukifanya vitu kwa namna ya tofauti, basi ni wazi kuwa unaenda kupata matokeo ya tofauti na vile wengine wanapata. Sasa hapa kuna njia ambayo unaweza kutumia ili kuweza kupata matokeo yasiyo ya kawaida.

 

Kwanza, ni kuhakikisha kamba unafanya kazi kwa bidii. Unaweza ukawa hauna kipaji cha kutosha kulinganisha na watu wengine, unaweza ukawa hauna konekisheni za maana ukilinganisha na watu wengine. Unaweza ukawa hujazaliwa kwenye familia ambapo kila kitu kimeshapangwa kwa ajili yak o ili uweze kukipata. Ila hata kama hauna bahati ya kuwa na hivyo vitu vyote, bado kuna kitu kimoja ambacho unaweza kufanya. Na kitu hiki ni kufanya kazi kwa bidii kuliko mtu mwingine  yeyote. Kufanya kazi kwa bidii kuna uwezo mkubwa wa kukutofautisha wewe hapo na watu wengine na hivyo kukufanya uzidi kuwa kipekee kabisa

Kuna vitu katika maisha viko nje ya uwezo wako. Kwa mfano kipaji cha rafiki yako, mtaji na sapoti aliyonayo mshindani wako kwenye biashara au ukubwa na ujuzi wa watu wanaofanya nao kazi…. lla kuna kitu kimoja ni uhakika kuwa kipo ndani ya uwezo wako. Na kitu hiki ni kufanya kazi kwa bidii. Kufanya kazi kwa bidii hakuhitaji kipaji, rasilimali za kipekee, konekisheni wala mtaji mkubwa. Kufanya kazi kwa bidii ni kuweka kazi inapohitajika, basi.

 

Ngoja ni kwambie kitu. Kuanzia leo jiwekee utaratibu kwamba, bila kujali wengine wana konekisheni kiasi gani. bila kujali wengine wamesoma kwa kiwango gani au wana sapoti kiasi gani. jiwekee utaratibu kwamba hakuna mtu yeyote ambaye anaweza kufanya kazi kwa bidii kunizidi mimi hapa.

 

Ikumbukwe kuwa kufanya kazi kwa bidii sio kipaji. Kipaji kipo tu kukusaidia kuanza kufanya kazi ila kipaji pekee hakikupeleki kwenye NCHI ya AHADI. Ila ukifanya kazi kwa bidii, ni wazi kuwa utafika nchi ya ahadi

 

 

Pili ni nidhamu. Nidhamu kwenye kile unachofanya. Kuhakikisha kwamba unakifanya hata kama hujisikii kukifanya. Kuhakikisha kwamba uakifanya hata kama watu wengine wote wanakikimbia  ili kukifanya kitu hicho kwa muda huo.

 

Tatu ni kuheshimu vitu vidogo. Ujue vitu vidogo ndivyo huwa vinapelekea kupata vitu vikubwa. Hata hivyo, watu wengi huw wanadharau vitu vidogo huku wakiwa wanasubiria vitu vikubwa. ukweli ni kwamba huwezi kupata vitu vikubwa kama umeshindwa kutumia vizuri vitu vidogo. Ukiwa mwaminifu kwenye mambo madogo ni wazi kuwa utakuwa mwaninifu kwenye mambo makubwa pia. Kwa hiyo, unapaswa kuanza kuheshimu vitu vidogo ambavyo unakutana navyo siku hii ya leo. Badala ya kuishia tu kusema kwamba ungependa kupata milioni. Anza kuitengeneza ya kwako kwa kuweka akiba ya kiasi fulani ambacho wewe mwenyewe unapata. Badala tu ya kuishia kusema kwamba utaandika kitabu, jiwekee utaratibu wa kuhakikisha kwamba unaandika ukurasa mmoja kila siku kwa siku saba za wiki bila kukosa. Ni kwa jinsi hiyo utakuwa na uwezo wa kupata makubwa zaidi maana unakuwa unatumia vizuri vitu vidogo.

 

Nne, Kuwa na sababu za kwa nini unapaswa kufanikiwa. Sababu zako za kufanikiwa ndizo zinapaswa kukusukuama wewe kuweza kufaninisjha malengo yako na kila kit uambacho umejiwekea. Kamwe usikubali kurudi nyuma hata kidogo.

 

Tano, kuwa na malengo ambayo unayafanyia kazi kila siku. Bila kuwa na malengo, utapoteza mwelekeo. Badala yake kuwa na malengo ambayo

 

Rafiki yangu, hiyo ndivyo vitu vitano vitakavyokufanya uweze kufanikiwa na kushinda kwa kishido kwenye kazi zako. kila la kheri

Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

 Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391

Kutengenezewa blogu yako kitalaamu tuwasiliane kwa 0755848391

kila la kheri
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X