Fikra Tano Zinazokufanya Uzuie Mafanikio Makubwa


Habari ya siku ya leo rafiki yangu. Hongera sana kwa zawadi ya siku nyingine. Leo hi nimeona nikushikirikishe fikra tano ulizonazo Sasa hivi ila zinakukwamisha. Kama utaendelea na fikra hizi hasa kwa mwaka mpya 2021, utazuia mafanikio makubwa kuja kwako.

Fikra ya kwanza ni were kufikiri kuwa mafanikio yapo kwa uhaba. Yaani, kwamba mtu mmoja akifanikiwa basi wewe hautafanikiwa. Kiufupi, mafanikio hayapo kwa uhaba. Mwingine akifanikiwa na wewe utafanikiwa pia.

Fikra ya pili ni wewe kufikiri kuwa u mnyonge. Najua wengi wamekuaminisha kupitia kauli na misemo mbalimbali kuwa wewe ni mnyonge. Ninachopenda kukwambia ni kuwa wewe hauna unyonge wowote ule. Huo unyonge ulionao umeusababisha mwenyewe. Una uwezo wa kufanya makubwa kuliko hata unavyofikiri.

Fikra ya tatu ni wewe kuamini kuwa huwezi bila ya msaada wa mtu fulani. Tena unakuta unalalamika sana pale ambapo mtu mwingine anakuwa hajakusaidia au kukupa kitu. Unaanza kusema ningekuwa mbali kama asingekuwa mjomba au shangazi AMBAYE amekataa kunisaidia mtaji, konekisheni au rasilimali fulani.  Japo muda mwingine unachoongea kinaweza kuwa sawa, ila wewe unapaswa kuudhihirishia ulimwengu kuwa kweli unastahili kupewa kitu fulani. Na kweli kama unastahili kupata hicho kitu ni wazi kuwa hutakwama. Hata kama mjomba au shangazi atakataaa kukusaidia basi atatokea mtu mwingine wa kukuinua.

Fikra ya nne ni wewe kufikiri kuwa kipaji chako ni kwa ajili yako. Hivyo, unaweza kukitumia au la ukaacha kukitumia. Huwa napenda kusema kuwa kipaji siyo chako, Bali ni Cha jamii. Kadiri unavyotumia kipaji chako kuisaidia jamii ndivyo na wewe unaendelea kunufaika ZAIDI. Kwa mfano,mwanamuziki anatumia kipaji chake kuimba na kuburudika na kadiri amavyoumtumia kipaji chake ndivyo watu wengi wengine wanavyonufaika kwa kusikiliza nyimbo zake na yeye pia ananufaika. Unaweza kukuta mwanamziki anamhitaji mwanamziki mwingine kuburudika. 

Kumbe usiache kutumia kipaji chako, ulimwengu unakihitaji.

Fikra ya tano ni fikra inayokusukuma wewe kusubiri kila kitu kiwe sawa ili uweze kuanza. Kiufupi, hata kama mambo hayajakaa sawa, bado Kuna kitu ambacho unaweza kuanza kufanya ili kufanya mambo yakae sawa 

Rafiki yangu, hizo ndizo fikra Tano ambazo kama itaendelea nazo, Basi zinakukwamisha sana ndani ya mwaka 2021. Nakutakia maandalizi mema ya mwaka mpya 2021. Kila la kheri.

Kesho Yako Iko Mikononi Mwako

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X