IPAMBANIE KESHO YAKO


 

Siku moja Arnord Shwarzenegger alikuwa akihadithia jinsi alivyopata ajali na kutoa damu wakati wanaendelea kurekodi tamhiliya. Kwa hali ya kawaida ya ubinadamu kila mtu alimwonea huruma na hasa director wake na hivyo alitaka wasitishe hilo zoezi la kurekodi tamhiliya ili Arnold aende hospitali kutibiwa kwanza.

Lakini Arnold Shwarzenegger alikataa. Alisema, “nimekuja hapa kurekodi tamhiliya na sitaondoka hapa mpaka kilichonileta kiwe kimekamilika. Hili tukio linaenda kuongeza uhalisia kwenye tamhiliya yetu”. Alihitimisha.

Kitu hiki kimenifanya nikumbuke maneno ya kuwa *ukitoa jasho jingi wakati wa mazoezi, utatoa damu kidogo wakati wa vita* .

Kumbe

1.  Kuna wakati unapaswa kuamua kujituma na kuumia kwa ajili ya kesho yako. 

2. Unapaswa kuachana na raha za muda mfupi kwa ajili kesho yako.

3. Unapaswa kuachana na visingizizio vinavyokuzuia kuifikia kesho yako.

Kwenye sehemu ya tatu ya kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO. Nimeeleza kuhusu Arnold Schwarzenegger na masomo muhimu ya kujifunza kutoka kwake. Pata nakala ngumu leo kwa shilingi 20,000 tu.

Wasiliana nami Sasa kwa 0755848391

Kesho Yako Ipo Mikononi Mwako


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X