JINSI YA KUOMBA FEDHA KUTOKA KWA WATU WENGINE: Njia Sita Zilizothibitishwa na Zisizoshindwa


 

Walau kila mtu aliyekuzunguka ana kiasi fulani cha fedha ambacho yupo tayari kukitumia. Kuna mtu unaweza kuwa naye na akawa anakwambia kuwa hana fedha hata kidogo. Lakini wakati mnaendelea na maongezi, kinaweza kupita kitu fulani ambacho mtu huyo anapenda na mtu huyo akawa tayari kukilipia. Sasa unaweza kujiuliza, hivi kweli mtu huyu hakuwa na fedha au alikuwa anatania?

Kuna wakati, watu huwa wapo tayari kujikopa ili tu watumie fedha kupata kitu fulani. Sasa leo ninaenda kukufundisha njia za kuomba fedha kwa watu, zitakazokuwezesha kupata fedha kirahisi kutoka kwa watu na kuzivuta kuja kwako.

1. Kuwapa Watu Kitu Wanachotaka

Zig Ziglar ambaye ni mhamasishaji maarufu wa Marekani amewahi kunukuliwa akisema kuwa, unaweza kupata unachotaka kama utawasaidia watu kiasi cha kutosha kupata kile WANACHOTAKA. Kwa hiyo na wewe muda wote unapaswa kujiuliza hivi watu wanataka kitu gani? Ukigundua kitu ambacho watu wanataka na ukawa tayari kuwapa watu kitu hicho, ni wazi kuwa watu hao watakuwa tayari kukupa wewe fedha. Na hiyo rafiki yangu ndiyo njia ya kwanza ya wewe kuomba fedha kwa watu. 

2.  Kutatua Matatizo Na Changamoto Zinazowakumba Watu.

Matatizo na changamoto yanayokumba watu, vinapaswa kuwa FURSA kwako. Ukiweza kutatua tatizo ambalo unaona wazi kuwa linawakumba watu waliokuzunguka, watu haohao watakuwa tayari kutoa fedha zao mfukoni ili wakupe wewe. Kwa mfano, mtu yupo tayari kutoa kiasi cha fedha mfukoni ili kununua vocha. Kwa nini? Kwa sababu anajua akinunua vocha itamsaidia kupata muda wa maongezi, sms au Mb za kuperuzi mtandaoni.

 Hivyo, vocha inatatua tatizo lake la kuwasiliana na watu. Vocha inawafanya watu wa mbali wasogee karibu na watu wapo tayari kutoa fedha mfukoni ili kuipata. Na hiyo hapo rafiki yangu, ndiyo njia nyingine ambayo na wewe unaweza kuitumia kuomba fedha kwa watu.

3. Kuanzisha Biashara Na Kuwaita Watu Wawekeze.

Kuna watu wenye mawazo mazuri ila hawana fedha ya kuwasaidia kuanzisha biashara. Na kuna watu wana fedha ila hawajui waifanyie nini. Sasa kama wewe una mpango mzuri wa kibiashara unaweza kuongea na watu na kuwelekeza watu kuhusu wazo lako la kibiashara na watu hao wakawa tayari kukupa fedha kutoka mfukoni mwao ili uanzishe biashara. Hiyo nayo rafiki ndiyo ni njia nyingine ya kuomba fedha kutoka kwa watu.

4. Kuongeza Thamani Yako.

Unalipwa kulingana na thamani yako. Kadiri thamani yako inavyokuwa kubwa, ndivyo watu wanakuwa tayari kukulipa zaidi wewe. Hivyo, mara zote  kazana kuongeza thamani yako kadiri uwezavyo ili watu waweze kuendelea kutoa viwango vikubwa vya fedha mfukoni mwao, kukupa wewe.

Mfano mzuri wa hili tunaweza kuliona kwa wachezaji wa mpira. Wachezaji wote huwa wanacheza kwa dakika 90 uwanjani. Ila kati ya hao kuna wachache ambao huwa wanalipwa kiwango kikubwa cha fedha na wengine kiwango kidogo. Kwa nini, baadhi ya wachezaji walipwe kiasi kidogo na wengine walipwe kiwango kikubwa wakati wote wanacheza dakika 90 tu. Jibu ni kwamba kuna wachezaji ambao thamani yao ni kubwa ukilinganisha na wengine. Hivyo, na wewe ukitaka kulipwa zaidi,basi ongeza thamani yako.

Na thamani yako unaweza kuiongeza katika eneo lolote lile. Kubuni kitu ambacho watu wanahitaji.

Watu wanaweza kuwa wanahitaji kitu fulani ila wakawa hawajui kama wanakihitaji hicho kitu. Hiki ndicho kilitokea miaka kadhaa nyuma. Watu walikuwa wanahitaji simu janja (smartphone) ila walikuwa hawajui kama wanazihitaji. 

Lakini Steve Jobs aliliona hilo na kuamua kuitengeneza kwanza. Tangu  zilipoanza kutumika, watu hawataki kuacha kuzitumia tena. Kila mtu anapenda apate simu hizo na awe nazo nyingi zaidi.

Na hiyo rafiki yangu, ndiyo nyingine ya kuomba fedha kutoka kwa watu.

KUJIFUNZA ZAIDI JIPATIE NAKALA YA KITABU CHA MAAJABU YA MTANDAO WA INTANETI KWA KUBONYEZA HAPA

6. Kuwafanya wateja waje kununua zaidi kwako 

Wateja wako wa Sasa hivi ni watu muhimu sana kwako. Sasa kitu kikubwa unachoweza kufanya ni kuwavuta ili waje kwako. Na utaweza hili kwa kutoa huduma bora. Mteja asinunue kwako mara moja tu. Badala yake, mfanye aendelee kununua na kununua tena. Unaweza kujifunza zaidi kuhusu hili kwa kusoma kitabu changu cha MAMBO 55 YA KUZINGATIA KABLA YA KUANZISHA BISHARA kwa kubonyeza HAPA. Hiyo  rafiki yangu, ni njia nyingine ya kuomba fedha kwa watu.

7. Kuuza Kitu Kwa Mtu

Ujue tunaishi katika dunia ambayo mauzo ni kitu cha muhimu sana. Unaweza kuishi ndani ya siku bila ya kuhitaji uwepo wa mwanasheria au daktari. Lakini huwezi kuishi ndani ya siku bila uwepo wa mtu wa mauzo. 

Chakula unachokula, ni kwa sababu yupo mtu anayeuza. nguo ulizovaa ni kwa sababu kuna mtu anauza. Hivyo, na wewe jifunze mauzo. Chukua kitu chochote ukauze. Hata kama ni kalamu, gari, tunda au ujuzi wako. Ila uza kitu ili uweze kupata fedha. Na mara nyingi utapaswa kuuza kwa bei ambayo wewe mwenyewe unapata faida au cha juu kidogo. 

Hiyo rafiki yangu ni njia nyingine ya kuomba fedha kutoka kwa watu.

Rafiki yangu, hongera sana kwa kujifunza njia hizi Saba zisizoshindwa za kuomba fedha kutoka watu wengine. Nikitakie Kila la kheri kwenye kuweka kwenye vitendo hiki ulichojifunza. Umekuwa nami, 

Godius Rweyongeza


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X