Juzi asubuhi nilikuwa namwagilia kwenye bustani yangu. Nyuma yangu kulikuwa ndege aina ya yangeyange kama kumi hivi. Sikuwa na muda nao maana wao walikuwa wanaendelea na biashara zao na mimi nashughulika na yangu. Nikiwa naendelea walitokea yangeyange wengine ambao walikuwa kama ishirini hivi. Wale waliokuwa nyuma yangu nao waliruka na kuungana na wenzao wakielekea mashariki kutoka nilipokuwa, ghafla waligeuka kuelekea kusini kwa pamoja. Kwa wakati huu nilikuwa sasa nikiwafuatilia kwa umakini mwenendo wao. Maana kwa siku nyingi (hata kabla ya juzi) nilikuwa nikijiuliza, hivi huwa inakuwaje ndege wanaelekea kwa upande mmoja kwa wakati mmoja,wanageuka kwa pamoja na kutua kwa pamoja.
Kwa muda mfupi ilinipasa kutafakari hayo ila kitu kimoja ndicho kilinifanya nitafakari zaidi. Na kitu hiki ni kwamba
Wakati yangeyange wanafanya mbwembwe zao za kuruka kuelekea mashariki, halafu kusini na hatimaye kurudi nilipokuwa. Kulikuwa na mwewe AMBAYE hapo mwanzoni alikuwa anaelekea upande wa mashariki kama yangeyange. Ila yangeyange walipogeuka kuelekea kusini hakugeuka, na bado yangeyange walipogeuka kurudi nilipokuwa hakugeuka. Yeye muda wore aliendelea kuelekea mashariki.
Hili lilinifanya nitafakari mengi. Hivi kweli in maana huyu mwewe hakuona hizi mbwembwe zote za kware. Kwa nini hakusimama kufuatilia walichokuwa wanafanya. Pengine hiyo ndiyo ilikuwa njia ya kware kupiga umbea. Mbona huyu mwewe hakuusikiliza huu umbea .
Hapo ndipo nilipojifunza masomo makubwa ambayo leo ninaenda kukushirikisha.
Kwanza nilijifunza kuwa bize na mambo yangu na kuachana na mengine.
Pia nilijifunza kuwa unapokuwa unajua wapi unaelekea huwezi kuteteleka na pale unapokutana na kitu Cha kukukwamisha njiani.
Hayo ndiyo mambo mawili niliyojifunza bila shaka na wewe utajifunza kitu hapa. Niambie umejifunza nini kwa kuweka maoni yako hapa chini