Siri Tano Zitakazokuwezesha Kufanikisha Malengo Makubwa 2021


 

Hiki ni kitabu changu bora Cha mwaka 2020. Anasema Mary

Leo nimeikumbuka hadithi ya Anne Lamott. Kwenye kitabu chake cha  Bird by Bird ameeleza JINSI siku moja alivyokuwa amepewa kazi ya kuchora ndege wengi kama  kazi ya nyumbani kutoka shuleni.

Alipofika nyumbani, aliona michoro ni mingi na hivyo akawa ameikatia tamaa. Lakini baba yake alimtia moyo na kumwambia, kama unataka kufanikisha hili unapaswa kuchora ndege mmoja baada ya mwingine (Bird by Bird). Na kweli alipoanza kuchora ndege mmoja baada ya mwingine, kila kitu kikakaa sawa.

Hili pia ndilo linapaswa kufanyika kwa ndoto na malengo yako makubwa. Kama una ndoto kubwa, anza kuifanyia kazi hatua kwa hatua. Mwisho wa siku ukiunganisha hizi hatua ndogondogo utakuta kuwa zimekuwa hatua kubwa sana.

Kama uliweka lengo kubwa mwanzoni mwa mwaka huu na ukasubiri lengo hilo litimie mwishoni mwa mwaka, yaani tarehe 31 ya mwezi huu. Ni wazi kuwa lengo Hilo halijatimia. Ila kama ulilifanyia kazi kidogokidogo ni wazi utakuwa umefika mbali.

Kwa hiyo kutokana na hadithi hii ya Anne Lamott ninaenda  kukupa siri tano za kipekee zitakazokusaidia kufanikisha malengo makubwa ndani ya mwaka 2021. 

Jipatie nakala hi kwa sh. 20,000 tu.

Na siri hizi ni kwamba, kama unataka kufanikisha malengo makubwa

 1. Anza kwa kuyafanyia kazi kidogokidogo

2. Endelea kulifanyia kazi lengo bila kuchoka.

3. Usisubiri mpaka mwisho wa mwaka ili uanze kufanyia kazi lengo lako, Anza Sasa. 

4. Ukipata ushauri mzuri, ufanyie kazi kama ilivyokuwa kwa Anne Lamott

5. Ukiona unalalamika kwa nini hutaweza kufanikisha lengo lako, ujue hujafikiria nje ya boksi, maana siku zote penye nia pana njia.

Jipatie nakala ya kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO ili ujifunze  na mbinu sahihi zitakazokuwezesha kufanikisha NDOTO ZAKO.

Gharama ya nakala ngumu ya kitabu ni 20,000/- tu


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X