Mwaka 2020 unaelekea kuisha. Umekuwa ni mwaka wenye matukio mengi sana ndani yake. Kuna watu waliweka malengo mwanzoni mwa mwaka ila hawakuanza kuyafanyia kazi, wakisubiri mpaka katikati mwa mwaka. Baadaye ulitokea mlipuko wa ugonjwa wa Corona. Watu waliendelea kuhairisha zaidi malengo mpaka Corona iishe. Baadaye ulifuata uchaguzi mkuu. Nao uliwafanya watu wengi wamezwe kwenye siasa huku wakihairisha malengo yao. Sasa mwaka ndio umefikia ukingoni na watu bado hawajafanikisha malengo yao. Wengine walioweka malengo mwanzoni mwa mwaka hata hawakumbuki kabisa kama waliweka malengo fulani mwanzoni mwa mwaka. Walioandika hata hawakumbuki waliandika wapi malengo hayo. Wakati ambao hawakuyaandika ndio kabisa hata hawana habari wala hawakumbuki kama waliwahi kuwa na malengo mwaka huu.
Sasa ndoto na malengo unavyopaswa kufanyia kazi 2021 vinaweza kufanikiwa au kutofanikiwa. Vifuatavyo ni vitu ambavyo vinaweza kukuzuia kufanikisha malengo na ndoto zako mwaka 2021
1. Kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja.
Najua wazi kuwa Kuna mambo mengi ambayo ungependa kufanikisha ndani 2021. Lakini haya yote hupaswi kuanza kuyafanyia kazi kwa wakati mmoja. Chagua walau malengo matano makubwa ambayo utayafanyia kazi mwakani, kisha kwenye hayo malengo yape kipaumbele, jua lengo gani linapaswa kuwa la kwanza, lipi linapaswa kuwa la pili n.k. Baada ya hapo anza kufanyia kazi lengo moja Baada ya jingine. Usikimbizane na kila lengo kwa wakati mmoja. Ukiyafanyia yote kazi kwa wakati mmoja utafeli kwa sababu ya kugawa rasilimali zako. Kwa hiyo ili mwaka wako uwe wa mafanikio makubwa hakikisha unafanyia kazi lengo la kwanza na kulikamilisha kisha uende kufanyia kazi lengo linalofuata.
2. Kujithibiti.
Utashindwa kufanikisha malengo yako mwaka 2021 kama hutaweza kujithibiti. Kwa mfano unapaswa kuthibiti tamaa ya kutumia fedha hovyo. Unapaswa kujithibiti hasa katika masuala ya muda na kuhakikisha unautumia vizuri na kwa mambo yenye manufaa. Kiufupi, jitahidi kadiri uwezavyo kuhakikisha kuwa unathibiti tabia zako zote mbaya ili ubaki na tabia zitakazokuwezesha kupata mafanikio makubwa.
3. Kupunguza marafiki
Marafiki wanaweza kupelekea wewe ufanikishe malengo yako au usiyafanikishe kabisa. Marafiki wanaweza kukuvuta chini na kukufanya ukate tamaa au wanaweza kukusukuma ufanikishe malengo yako. Naomba sana, ujitahidi kuwa ma marafiki wachache ila wenye maono makubwa na ambao watakusaidia wewe kufanikisha malengo yako mwaka 2021.
4. Kusubiri kila kitu kikae sawa
Kama utasubiri kila kikae sawa ili uanze kufanyia kazi malengo yako mwaka 2021, utasubiri sana. Maana haitatokea eti mazingira na kila kitu kikajipanga kwa ajili yako. Badala yake, wewe ndiye unapaswa kuamua kupangilia mipango yako na kuanza hata kama mambo mengine hayajakaa sawa. Anza kufanyia malengo yako hata kwa udogo, Anza kufanya kitu kidogo kitakachokupelekea kufanikisha malengo yako.
Jipatie nakala ya KITABU cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO na KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI ili upate vitabu viwili vyenye mwongozo kamili wa kukusaidia wewe kufanikisha malengo na ndoto zako. Tuma ujumbe au piga kwa 0755848391 ili upate vitabu hivi.
5. Kusubiri mpaka dakika ya mwisho ili ufanye kazi.
Kama kuna kitu kitakukwamisha ni wewe kusubirisha shughuli za muhimu kufanyika mpaka siku ya mwisho. Kitu hiki kimethibitika kuwa ni chanzo cha watu wengi kufanya kazi hovyo. Kwa mfano mwanafunzi anapokuwa anajua kuwa anapaswa kusoma ila akasubiri mpaka siku ya mwisho asome, atajikuta siku za mwisho anasoma kwa msongo sana, kitu kitakachopelekea ufaulu wake uwe wa hovyo pia.
Hivyo hivyo kwa watu walio kazini wanapokuwa na majukumu ya kikazi ila wakayahairisha mpaka siku nyingine, wanakuta siku ya kuanza kazi imefika ila kazi hawajafanya, hivyo wanaishia kuifanya hovyo.
Kwa hiyo, kwa majukumu yako yote ambayo utapaswa kuyafanya, basi yafanye kwa wakati bila kusubiri siku ya mwisho. La sivyo utashindwa kutimiza malengo yako 2021.
Makala hii itaendelea.
Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA
Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA
Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA
Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391
Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI na kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391
Kutengenezewa blogu yako kitalaamu tuwasiliane kwa 0755848391
kila la kheri
One response to “Vikwazo vitano vitakavyokuzuia KUFIKIA NDOTO ZAKO ndani ya 2021”
[…] Juzi niliomba watu wapendekeze mada ambazo nitaandikia kwenye blogu yangu kupitia status yangu ya whatsap. Nilipokea maombi kadha wa kadha ambayo nitakuwa nayafanyia kazi moja baada ya jingine. Ombi mojawapo lilikuwa ni kuandika makala maalumu kueleza kwa nini watu wanashindwa kufikia NDOTO zao. […]