Vitu Vitano Kutoka Kwenye Kamusi Ya Watu Wa Kawaida; Viepuke Kwa Manufaa Yako


Nakala za kitabu hiki, zipo (tuwasiliane kwa 0755848391)

Watu wote ambao huwa wanaishi maisha ya kawaida huwa wana vitu ambavyo huwa vinawaunganisha. Na vitu hivi huanzia kwenye fikra zao, jinsi wanavyoishi maisha yao ya kila siku,ongea yao na hata ulaji. Muunganiko wa vitu hivi vyote ndiyo huwafanya wawe na maisha ya kawaida. Vitu hivi ndivyo huwafanya waendelee kuvuta umasikini kwao na hata kushindwa kufanikisha mambo makubwa maishani mwao. Hivyo, siku ya leo nimeona nikuelezee vitu ambavyo watu wa kawaida huwa wanafanya, vitu hivi ndivyo huwafanya waendelee kuwa na maisha mabovu, kuvuta umasikini na hata kuvuta magonjwa. Kwa hiyo, viepuke vitu hivi kwa manufaa yako ili uweze kuwa na maisha bora, uweze kuvuta utajiri na afya bora pia.

 

Kitu cha kwanza ambacho watu wa kawaida hufanya ni kufanya kila kitu kama ambavyo kila mtu anakifanya

Yaani, hakuna kujitofautisha wala kufanya kitu cha kipekee. Kwenye kamusi ya watu wa kawaida kujitofautisha ni kama dhambi. Hivyo, kila mtu anapigana kuhakikisha kwamba anakuwa kama mwingine. kiufupi tunaweza kusema kwamba watu wa kawaida wote wanapaswa kufanana kama vitumbua.

 

Rafiki yangu kama unataka kuishi maisha mazuri, kuliishi kusudi lako na kuacha alama hapa dunaini, huna budi kuhakikisha kwamba unaachana na maisha ya kawaida ambayo kila mtu anayaishi. Badala yake unapaswa kufanya vitu kwa utofauti ili upate matokeo ya tofauti.

Kitu cha pili ambacho kinawatambulisha watu kawaida ni kujua kila kitu

Kwenye kamusi ya watu wa kawaida, hakuna kitu kinaitwa kujifunza na kuongeza maarifa. mtu wa kawaida anajua kila kitu. Kwake kujifunza ni kupoteza muda. Yeye hataki kusoma vitabu wala kujifunza, anasubiri aje asomwe siku za mbeleni. Hiyo ndiyo kamusi ya watu watu wa kawaida inavyosema.

Hata hivyo, kwenye hali ya kwaida kama wewe unataka maisha ya mafanikio na kuondokana na maisha ya kawaida basi utapaswa kuhakikisha kwamba unajiwekea utaratibu wa kujifunza na kusoma vitabu kila siku. Dunia inabadilika kwa kasi sana kiasi kwamba usipobadilika na kujifunza kila siku, unaenda kupitwa na wakati. huo ni ukweli usiokuwa na upinzani.

Unaweza kujipatia nakala yangu ya kitabu cha MAAJABU YAKUSOMA VITABU kwa kubonyeza HAPA ili uweze kujua maajabu yaliyo kwenye usomaji wa vitabu. Au nitumie ujumbe wa whatsap kwa 0755848391

 

Kitu cha tatu kutoka kwa watu wa kawaida ni kuwa usitumie kipaji chako.

Kamusi ya watu wa kawaida inasema kwamba masuala ya vipaji waachie tu wazungu, huwezi kuongelea mambo ya vipaji barani Afrika ambapo wewe unahangaika kutafuta mlo wa siku. Kwa hiyo, kitu kikubwa ni wewe kuhakikisha kwamba umepata chakula cha kula siku hiyo tu, basi mambo mengine unaachana nayo.

Kama unataka kuishi maisha ya kawaida, fanya kama ambavyo watu wa kawaida wanafanya. Hata hivyo, kama unataka kuishi maisha ya tofauti, hakikisha unajitofautisha kwa kuanza kunoa kipaji chako. Tumia kipaji chako, maana kipaji kinakusaidia kufanikisha mengi maishani.

Kujifunza zaidi kuhusu jinsi ya kugundua kipaji chako, kukinoa na kukiendeleza basi jipatie nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI, Nitumie ujumbe au piga kwa namba 0755848391 au bonyeza HAPA ili kupata nakala laini

 

Kitu cha nne kutoka kwa watu wenye maisha ya kawaida ni kuwa maisha ni leoleo, kila unachopata tumia.

Kwenye kamusi ya watu wa kawaida hakuna kitu kama kuwekeza, kuweka akiba, kuiandaa kesho yako n.k. wao wanachojua ni kwamba leo ni leo asemaye kesho ni mwongo. Hivyo, hata kama mtu anapokea fedha, kitu cha kwanza kabisa anachofanya ni kutumia kiasi chote cha fedha kwa pamoja bila ya kuchelewa.

Ifahamike kwamba leo una nguvu ila kesho inakuja ambapo uzee  utakunyemelea. Hivyo, unapaswa kujiandaa kwa ajili ya nyakati zijazo. Usiwe kama nyani ambao kila wanapopata wanakula na kuondoka, huku wakidhani kwamba kesho watakuta chakula kingine na kula. Maisha ni mipango na hiyo mipango unapaswa kuiweka wewe mwenyewe.

Kitu cha tano kutoka kwa watu wa kawaida ni kwamba unapaswa kufanya vitu kwa namna ile ile kila siku.

Kamusi ya watu wa kawaida inasema kwamba, unapaswa kufanya vitu kwa namna ile ile kila siku. Ulichofanya jana ndicho unapaswa kurudia tena kufanya leo na ndicho utafanya kesho. Hivyo, hakuna kwenda hatua ya ziada, hakuna kujituma zaidi wala kufikiri nje ya boksi.

Na wewe ukiendelea kufanya hivi, nakuhakikishia utaendelea kupata matokeo yaleyale ambayo umekuwa unapata siku zote. Sheria inasema kwamba, kila kitu kitaendelea kwenye mwendo wake, mpaka pale nguvu ya tofauti itakapotokea kwenye kitu hicho. hivyo, ukiendelea kufanya vitu hivyo hivyo, utaendelea kulipwa kiasi cha fedha hicho hicho ulichokuwa unalipwa miaka nenda, miaka rudi. Tena kinaweza hata kupungua, ni mpaka pale utakapomua kwenda hatua ya ziada, kujituma, kufikiria njea ya boksi ndipo utaanza kupata matokeo ambayo hukutarajia.

 

Rafiki yangu, leo tumeona mambo kadha wa kadha kutoka kwenye kamusi ya watu wa kawaida. Yaepuke mambo haya ili uweze kuishi maisha mazuri nay a kipekee. Kila la kheri

Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

 Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI na kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391

Kutengenezewa blogu yako kitalaamu tuwasiliane kwa 0755848391

kila la kheri



Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X