Vitu Vitano Unavyopaswa Kuzingatia Kabla Hujaingia Ndani Ya Mwaka Mpya 2021


mwaka mpya 2021

Jana nilikuwa nasikiliza wimbo wa Ben Paul  unaoitwa Sikukuu. Hii ni kava ya wimbo zamani kidogo ulioimbwa na bendi ya Jobiso.

 Kwenye wimbo Kuna mstari unaosema miaka inaenda mbio.. 

Ndio ni ukweli kuwa miaka inazidi kusogea na kila siku inayopita ndiyo inazidi kupita.

Na mwaka huu hatimaye na sasa umefika mwishoni. Nakumbuka mwaka huu ulianza kwa mbwembwe nyingi, watu waliusubiri kwa kukesha na ilipofika saa sita baruti na mbwembwe nyingine zilipigwa.  Wapo ambao hawakulala kabisa usiku wa kuamkia mwaka huu.

Lakini Cha kushangaza watu hao hao walishindwa kukesha siku zilizofuafa kwa ajili ya kufanyia kazi malengo Yako. Na hiki ni kitu ambacho siku zote kinanishangaza kuona jinsi ambavyo watu wanakesha kuusubiri mwaka mpya ila wanashindwa kukesha kutimiza malengo yao. 

Tukiachana na hayo mwaka 2020 umekuwa na mambo mengi ndani yake ambayo yametokea na hasa ugonjwa wa Corona. Huu umekuwa kikwazo kwa vitu vingi, kitu ambacho kimepelekea watu wengine kusema mwaka 2020 tuufute. Ihesabike kuwa 2020 haikuwahi kutokea. Huku wengine wakiomba mwaka tu uishe ili mambo mengine yaendelee…

Sasa kwa leo kuna vitu ambavyo ningependa ufahamu kwa kina kabla mwaka huu haujaisha. Na vitu hivi vitakuwa msaada mkubwa kwako mwaka 2021 

1. Unapaswa kukesha mara nyingi ukifanyia kazi malengo hako kuliko unavyokesha kuusubiri, kuliko unavyokesha kutazama tamthiliya au kufuatilia mechi yoyote ile. Mwaka 2021 unapaswa kuanza kujenga mazingira ya wewe kutazamwa Kwenye runinga na siyo wewe unatazama wengine siku zote.

2. Unapaswa kuachana na tabia Yako ya kughairisha majukumu Unavyopaswa kutimiza. Timiza majukumu yako kwa wakati.

3. Unapaswa kuanzisha tabia ya kuamka mapema. Ni kitu Bora kwa afya Yako na malengo Yako pia.

4. Unapaswa kuachana na tabia ya kusikiliza na kupokea maoni hasi kama vile yamesemwa kwako. Mtu anapotoa maoni anakuwa aongelea hali husika ila siyo wewe. Kwa hiyo, uwe mwaka wako wa kwanza ambao hautaathiriwa na maoni hasi.

5. Unapaswa kuanzisha tabia ya kusoma na KUJIFUNZA.  Mwaka 2021 walau soma kitabu kimoja au viwili kila mwezi

Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

 Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391

Kutengenezewa blogu yako kitalaamu tuwasiliane kwa 0755848391

kila la kheri


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X