Acha leo ni kwambie kitu


 

Ujue ukifanya kitu kizuri watu watakuwa tayari kukiongea hicho kitu kwa watu wengine. Watu watakuwa tayari kuwashirikisha watu wengine kuhusu hicho kitu. Watu watakuwa tayari kufanya kila kitu kizuri kuhakikisha na wenzao wanajua hicho kitu kizuri.

 

Mfano ukiandika kitabu kizuri au ukiimba wimbo mzuri. Watu watakuwa tayari kuushirikisha huo wimbo kwawatu wengine , wengine watakuwa tayari kuuimba na kuucheza ili kuonesha kuwa huo wimbo wanaupenda. Kwa hiyo rafiki yangu siku zote hakikisha kamba unafanya kitu kizuri  maana kama wanavyosema wahenga, siku zote kizuri kinajiuza wakati kibaya kikiwa kinajitembeza.

 

Wakati huu nakumbuka Yesu alivyokuwa anafanya miujiza kwenye biblia. Alipokuwa anatenda miujiza alikuwa anawaambia watu kuwa wasiseme hicho kitu kwa watu wengine. Ila kilichokuwa kinatokea ni KWAMBA WALE WATU WALIKUWA WANAWAENDA KUONGEA KILEKILE ALICHOWAKATAZA.

ILAUKIFUATILIA KIUNDANI UNAGUNDUA  kwamba kilicho ndani ya hiki kitu ni kuwa watu wapo tayari kusema kitu kizuri kwa wengine. Kizuri kinajiuza.
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X