Ndugu wazazi, siku ya leo nimeona niongee nayi kitu kimoja tu kuhusu malezi na makuzi ya watoto hasa kwa upande mzima wa usomaji wa vitabu.
Ndugu mzazi nadhani inafahamika sana kuwa watoto huwa wananunuliwa midoli kwa ajili ya kucheza kadiri wanavyokua. Ila inashauriwa pia mzazi umununulie mwanao kitabu kama mdoli anapokuwa anakua. Hiki kitamsaidia kuanza kumjengea mazingira ya kuzungukwa na vitabu akiwa bado mdogo na hivyo kuanza kumjengea tabia ya kusoma vitabu mapema.
Badala ya kumununulia midoli yenye asili ya bunduki, unaweza hata kununua kitabu kimoja chenye picha mwanzo mpaka mwisho na mtoto akawa anafurahia kufunua na kuangalia picha. Kwa jinsi hiyo, ni wazi kuwa utakuwa umeweza kumjengea tabia nzuri ya kuanza kusoma mapema.
Hakikisha umefuatilia video hii hapa yenye NJIA 13 ZA KUWAFANYAWATOTO WAKO WAPENDE KUSOMA VITABU HAPA
USISAHAU PIA KUSUBSCRIBE
WASHIRIKISHE NA WENGINE