Kwa mwaka huu 2021 kuna kitabu kimoja ambacho nitasoma kuanzia Januari mpaka Disemba. Sio kawaida kwangu kusoma kitabu kwa muda mrefu kihivyo, ukizingatia kuwa huwa nasoma walau kitabu kila wiki. Ila kwa mwaka huu kitabu cha Peter Drucker kinachoitwa The Daily Drucker nitakisoma mwanzo wa mwaka mpaka mwisho.
Kukielewa kitabu hiki inabidi kwanza tumwelewe Peter Drucker mwenyewe. Huyu ni mwandishi wa karne ya 20 AMBAYE ameandika vitabu vingi kuhusu uongozi, usimamizi na uendeshaji wa biashara. Vitabu vimesaidia sana kwenye biashara na vimetumiwa na viongozi wakubwa kwenye biashara akiwemo Jack Welch, alitewahi kuwa mkurugenzi wa kampuni kubwa ya GE.
Sasa kumbe kiufupi unaweza kuona kitabu hiki ni cha aina gani. Ni kitabu chenye mkusanyiko wa mafunzo mafupi 365 kutoka kwa Peter Drucker kuhusu biashara na usimamizi wa biashara. Nitakuwa nikisoma kitabu hiki kila siku kwa mwaka mzima.
Kila siku kwenye mwaka kuna andiko fupi kulingana na siku husika.
Sambamba na hilo, mwaka huu nitasoma kazi nyingine za mwandishi huyu. Huu utakuwa mwaka wangu wa kwanza kusoma kazi zake. Hivyo, nitaendelea kukupa mrejesho kadiri nitakavyokuwa nikizisoma.
Rafiki yangu hicho ndicho kitu ambacho nimeona nikushikirikishe kwa siku ya leo. Pengine na wewe una kitabu chako utakachosoma mwaka huu. Naomba kujua ni kipi.
Karibu sana.
Kupata nakala ya kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO tuwasiliane kwa 0755848391