JINSI YA KUIBADILI DUNIA: Vitu Saba Vya Kufanya Kama Unataka Kuibadili Dunia


Jana karibia kwenye kila mtandao yote ya kijamii, habari iliyoshika vichwa ilikuwa ni bilionea mpya kwenye nafasi ya kwanza, Elon Musk. Video na makala nyingi ziliandikwa kuhusu bilionea huyu. Ila ukiangalia haya yote yaliyoandikwa, unapata kitu Kimoja kikubwa kutoka kwa bilionea huyu. Na kitu hiki ni kuwa  ANAIBADILI DUNIA. Anaibadili kwa vitu anavyofanya na kuifanya kuwa bora zaidi huku akiwa na mpango wa kupeleka binadamu kwenye sayari mbalimbali na kutengeneza makazi huko. Sasa najua na wewe utakuwa unapenda kuibadili dunia, yafuatayo ni mambo matano unayoweza kufanya ili kuibadili dunia.

1. Kuwa wewe. Ngoja nikwambie, ukijaribu kuwa Elon Musk, Jeff Bezos au Bill Gates, utashindwa Sana. Ila ukiwa wewe utafanya makubwa. Kwa hiyo siri ya kwanza ya kuibadili dunia ni kuwa wewe.

2. Anza na kile ulichonacho, fanya kinachowezekana sasa, mwisho wa siku utaweza kufanya yasiyowezekana. Na hivi ndivyo Elon Musk alivyoeweza kufanya makubwa, ameanza na kile alichonacho mpaka kufika alipofika. Na wewe unaweza pia.

3. Siku zote shikilia ndoto yako kubwa bila kujali uko wapi au unapitia wapi. Elon Musk ameshikilia ndoto zake kubwa tangu akiwa mdogo nchini Afrika kusini miaka ya sabini na themanini mpake leo hii.

4. Inachukua muda kufikia mafanikio makubwa, hivyo jipe muda kufikia mafanikio makubwa pia.

5. Ukitaka kuonekana kwenye mitandao ya kijamii na kuuza sura, utaishia tu kuuza sura ila hutafanya kitu cha tofauti kwenye hii dunia. Ila ukitaka kuibadili dunia basi jifungue ndani fanya vitu vya tofauti ambavyo vinagusa maisha ya watu.

6. Jifunze Sana kwa kusoma vitabu maana siku zote vitabu ni lenzi ya kuona mbali. Vitabuvinekuwa pia ni lenzi kwa Elon Musk na mabolionea wengine.

7. Usiongee Sana. Acha kazi zako ziongee na kukutambulisha. Ebu fikiria ungekuwa wewe ndiyo umepata mabilioni yote hayo ya fedha. Ungefanyaje? Bila shaka siku ya jana ungeshinda mitandaoni unapiga picha na kuoost ila hali haikuwa hivyo kwa Elon Musk, aliandika maneno machache kisha akasema, back to work.

Hayo Ndiyo mambo saba yatakayokusaidia na wewe kuibadili dunia pia.

Sehemu ya pili kwenye kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO nimetoa mifano ya watu wanne ambao tunaeeza kujifunza kwao. Na Elon Musk nu mmoja wao. Sura ya 13 kwenye kitabu  hicho imemzungumzia yeye. Unaweza kupata nakala yako Leo hii. Tuwasiliane kwa 0755848391. Karibu.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X