JINSI YA KUIFANYA FAMILIA YAKO IPENDE KUSOMA VITABU


Rafiki yangu, hongera sana kwa siku hii ya kipekee Sana. Kama umekuwa unajiuliza ni njia gani ambayo unaweza kuitumia kuwashawishi wanafamilia kusoma vitabu ni wewe kununua vitabu na kuviweka kwenye mazingira ambayo yanaonekana kwenye familia.

Kadiri watu watakavyokuwa wanaona vitabu, itakuwa ni rahisi kwao kusoma kuliko pale ambapo huwa kinakuwa hakuna vitabu kabisa.
Kukiwa na runinga na tamthiliya, Ni wazi kuwa watu watakimbilia kuangalia runinga badala ya kusoma vitabu. Hivyo, anza kujenga mazingira ya kuweka vitabu hata kama ni kwa udogo

Kitu ambacho hupaswi kufanya Ni kumlazimisha mtu kusoma vitabu hata Kama unajua wazi kuwa vitabu hivyo vitmsaidia. Wewe soma na fanyia kazi vile unavyojifunza na watu wengine wataona kwako na hivyo kuiga kwako.

Kila la kheri
Godius Rweyongeza
Morogoro-Tz
0755848391


One response to “JINSI YA KUIFANYA FAMILIA YAKO IPENDE KUSOMA VITABU”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X