Kitu Kimoja Kitakachokukwamisha 2021


 

Rafiki yangu unaendeleaje. Watu wengi huwa wanaanza mwaka mpya kwa mbwembwe nyingi kwelikweli. Mwaka unapoanza watu wanaweka malengo makubwa na kuanza kuchukua hatua. Hata hivyo, huwa haichukui muda mrefu, watu hao huwa wanaanza kusahau malengo yao na kuanza kufanya kazi na vitu vyao kama walivyozoea. 

Na hata wale ambao huwa wanaendelea kufanyia kazi malengo yao huwa wanashindwa kuyatimiza kwa asilimia kubwa kwa sababu wengi huwa wanaanza mwaka kwa kufanya vitu vingi kwa wakati mmoja. Hiki kitu huwa kinawafanya watu wanaonekana wako bize sana, ila hawakamilishi chochote, mwisho wa siku watu hao wanachoka na hivyo, kumaliza mwaka wakiwa wameanza kufanya vitu vingi ila wakiwa hawajakamilisha chochote. Ninachokuomba ni kuwa jifunze kuanza kitu kimoja na kukikamilisha kwanza kabla ya kwenda kwa kitu kinachofuata. Hili litakusaidia sana kufanikisha makubwa na litakupa motisha ya Kufanikisha mambo mengi zaidi. Kiufupi kila unapokamilisha jukumu fulani unapata pia nguvu ya kufanya vitu vingine na kuvikamilisha pia.

Mwaka huu kuwa mtu wa Kukamilisha kila unachoanza hata Kama ni kidogo.

Kila la kheri.

Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

 Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391

Kutengenezewa blogu yako kitalaamu tuwasiliane kwa 0755848391

kila la kheri


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X