Madhara ya kuwa mzembe


 

Rafiki yangu, hongera kwa kupata nafasi ya kuiishi leo.  Hakikisha unaiishi leo kwa kufanya kazi kwa bidii, maana uzembe hauna faida yoyote ile maishani. Kufanya kazi kwa bidii kunalipa, tena kunalipa sana. 

Kwa leo sitaongelea faida za kufanya kazi ambazo najua ni nyingi sana na ninajua unazijua tu. Ila ninataka nikwambie hasara moja kubwa ya uzembe. Na hasara hii ni kuwa unadharauliwa na kila mtu hata mtoto mdogo. 

Looo! Kumbe uzembe sio dili hapa mjini. Kama unataka kufanya makubwa basi chapa kazi kwa bidii haswa. 

Kwenye kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO, nimeeleza moja ya sifa ya watu wanaofikia ndoto zao  kuwa ni kufanya kazi kwa bidii. Naomba ujitahidi kuhakikisha unapata nakala ya kitabu hiki, haswa Kama uko makini na ndoto yako kubwa.

Wasiliana nami sasa kwa 0755848391 jina ni GODIUS RWEYONGEZA.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X