Vitu Vitano Unavyopaswa Kufanya Ili Kufanikiwa 2021


 

Rafiki yangu kheri ya mwaka mpya kwako. Siku ya leo nimeona nikushirikishe vitu vitano ambavyo vitaufanya mwaka wako mpya uweze kuwa wa mafanikio makubwa sana

 

Kitu cha kwanza ni kuhakikisha kwamba unakuwa mvumilivu. Kuna usemi wa Warren Buffet naupenda sana. anasema kwamba kuna baadhi ya vitu kwenye maisha havihitaji haraka, huwezi kuwapa wanawake tisa mimba na ukategemea kupata mtoto ndani ya mwezi mmoja. Hii ndiyo kusema kwamba kama unahitaji mafanikio makubwa mwaka huu unapaswa kuyapa muda. Haupasi kukurupuka na kufanya kitu kimoja leo huku ukitegemea mafanikio makubwa kesho yake

 

Kama umedhamiria kuwekeza, usiwekeza mara moja leo na kusubiri uwekezaji wako huo ulete mafanikio makubwa siku ya kesho. Badala yake wekeza leo na endelea kuwekeza hata siku nyingine huku ukijua kwamba baada ya muda huo uwekezaji wako unakuja kulipa.

 

Pili hakikiasha kwamba unaongeza bidii kwenye kazi zako. ikumbukwe kwamba wewe ndiye mwenye ndoto kubwa na wala siyo mtu mwingine. Hivyo, hayo maono yako uliyonayo hata kama utakuwa unawashirikisha watu wengine hakikisha kwamba unaongeza bidii kwenye kuwashirikisha hao watu wengine maono yako ili na wao waweze kushiriki kile ulichonacho. Kiufupi kwa kila kitu utakachoamua kufanya hakikisha kwamba unakifanya kwa bidii.

 

Tatu, hakikisha kwamba kila mwezi unakuwa na jambo moja ambalo  utalifanyia kazi. ukifanyia kazi kitu kimoja kila mwezi, mwisho wa mwaka utajikuta kwamba umeweza kufanikisha mambo mengi sana.

 

Nne, usiongee sana. tenda sana

 

Tano, ukiamua kufanya kitu mwaka huu hakikisha unakifanya bila ya kurudi nyuma.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X