Hivi ndivyo unaweza kuonesha kuwa una upendo kwa watu


 

 

Ni njia gani unaweza kutumia kuonesha kwamba una upendo? Hivi umewahi kufikiria kuhusu hili?

Siku ya leo nimeona nikuoneshe njia ya kawaida ambayo unaweza kutumia kuonesha upendo kwa watu. na njia hii ni kuwasaidia watu  kufanya kitu fulani au kutimiza kitu fulani. Inaweza pia kuwa ni kuwasaidia watu kutatua tatizo fulani au hata kuwapa wazo ambalo linaweza kuwa msaada kwao.

 

Hiyo ndiyo njia ya kudumu ya kuonesha upendo wako kwa watu wengine. Na hii hata siku moja haihitaji wewe usubirie mpaka ifike siku ya valentine ili ufanye hivyo. Unaweza kufanya hivyo, mara zote na siku zote.

 

Ebu siku ya leo onesha upendo wako kwa watu kwa kufanya kitu kinachoonesha upendo kwao.

Angalia ni tatizo gani ambalo unaweza kuwasaidia kutatua

Angalia ni wazo gani ambalo unaweza kuwapa na likawa msaada kwao, angalia hata konekisheni ambazo unaweza kuwapa na zikaendelea kuwa msaada kwao. Kwa vyovyote vile, hakikisha kwamba unaonesha upendo leo. Na siku zote.

SOMA ZAIDI: Moyo Wako Uko Wapi?


Umekuwa nami,

Godius Rweyongeza
0755848391
KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA

HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA
Hakikisha umesubscribe kwenye YouTube Channel Yangu Ya Youtube Kwa Kubonyeza Hapa


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X