Inawezekana Kama Hautangalia Nyuma


 

Mhispania Hernán Cortés aliweka rekodi ya kipekee Sana alipoenda kupigana Mexico (Aztec) 

Kwanzaalienda kupigana na jeshi dogo (watu 600 tu).

 Pili, alipofika vitani alichoma meli zake moto na kuwaambia wanajeshi wake wote kuna uamuzi mmoja mkubwa uliobaki. Kushinda vita au kufa. Kwa hiyo, hakukuwa na njia nyingine ya kurudi nyuma maana alishachoma meli zake zote moto.

Linapokuja suala zima la mafanikio wengi wamekuwa wanashindwa kufanikiwa maana wanaamua kufanikiwa kwa mguu mmoja na mwingine unakuwa nyuma ukiendelea kufanya mambo yaleyale yanayowazuia kufikia mafanikio.  

Hivyo, wanapokutana na kikwazo jambo la kwanza linakuwa ni kurudi nyuma. Inawezekana kufanikiwa ila unapaswa kuchoma meli zako moto kwaza Kama alivyofanya Cortés.

Kuchoma meli moto maana yake nini? 

Ni uamuzi wa kuwa vitu vya nyuma umeamua kuachana navyo kabisa. Na Sasa unasonga mbele bila kurudi nyuma KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA. Yaani, kwamba ulikuwa unaishi maisha ambayo watu wengine wote walikuwa wanaishi, sasa unaamua kuanza kuishi maisha ya tofauti bila kujali kitu gani kitatokea. Hiyo ndiyo inaitwa FANYA AU KUFA (do or die).

Fanya kitu fulani mpaka uyafikie mafanikio makubwa au kufa ukiyaendea ila hakuna kurudi nyuma (no exit strategy).

Kama unaamua kuyaendea mafanikio makubwa huku ukiwa na mguu mmoja ndani na mwingine nje, utafeli haraka sana.

Ebu fikiria unaamua kuyaendea mafanikio makubwa huku ukiwa  

  • unaendelea kunywa pombe kila siku. Hiki kitu cha kukurudisha nyuma (exit strategy)
  • unaendelea kuvuta sigara 
  • unaaendelea kuwa na rafiki zako wabovu 
  • Unaendelea kula vyakula ambavyo havijengi mwili na wala hufanyi mazoezi 
  • Unaendelea kufanya vitu kwa namna ileile.

Kiufupi nipende tu kukwambia kuwa utajikwamisha mwenyewe tu.

Kwa hiyo fanya uamuzi wa kufanikiwa. Na wakati huohuo choma meli moto kwa

  •  Kuacha tabia zako zote mbaya 
  • Kumbatana na rafiki wazuri. Kama hauna Sasa ndio unakuwa muda wa kuwatengeneza. Vitabu pia vinaweza kuwa sehemu ya marafiki wazuri. 
  • Kuinuakipaji chako


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X