Inawezekana Kuinuka Tena Baada Ya Kuanguka


Kama hujawahi kuanguka maana yake hujawahi hata kujaribu. Ila kama umewahi kufanya au hata kujaribu basi unajua wazi kuwa kuna changamoto na vikwazo ambavyo huwa vipo katika safari yoyote ya kimafanikio. Muda mwingine katika safari kama hii unakuta umeanguka.

Hata hivyo, ninachopenda kukwambia ni kuwa unapaswa kuinuka hata baada ya kuanguka.

Ukianguka

1. Jiulize kitu gani kimesababisha uanguke. Unaweza kukuta labda ni kutokana na maarifa mabovu, au uamuzi ambao haukuwa sahihi, au ulichelewa kuchukua hatua, au pengine ulifanya mambo mengi kwa wakati mmoja kiasi kwamba hukuwekeza nguvu kwenye kitu kimoja.

2. Jiulize ni hatua gani unaweza kuchukua zikakuondoa kwenye hali Kama hiyo. Pengine ni kuachana na kufanya Mambo mengi na kufanya machache. Pengine ni kula kwa afya au hata kuachana na marafiki ambao wanakushawishi usifanye hicho kitu. 

3. Angalia ni rasilimali gani zilizopo unazoweza kutumia baada ya kuwa umepoteza kila kitu. Hapa ukiangalia vizuri, Ni wazi kuwa walau kutakuwa na kitu hata kidogo cha kukusaidia kuanzia.

4. Usiogope kuanza upya baada ya kuanguka. Kuanguka kwako ni ishara kuwa upo hai na Kuna vitu vikubwa unafanya.

5. Anza upya. Epuka  kurudia makosa ya zamani. Jifunze sana ili usije ukafanya makosa mengine makubwa.

Hivyo rafiki yangu ndivyo unaweza kuanza upya baada ya kuanguka.

, ,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X